Home Mchanganyiko MKUU WA WILAYA AMPONGEZA WEO KIHAGARA

MKUU WA WILAYA AMPONGEZA WEO KIHAGARA

0

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa bi Isabela Chilumba, akitoa salamu za Serikali katika kikao cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kepten John Komba mjini Mbamba-bay Wilayani hapa.pamoja na mambo mengine amewaagiza Madiwani hao kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wanajiunga kwa asilimia mia moja ifakapo Februari 29 mwaka huu.(Picha na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa).

**************************

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, amempongeza Afisa Mtendaji wa kata ya Kihagara Eva mayendayenda, kwa kuwarudisha shuleni watoto wawili waliokuwa wakitumikishwa kufanya kazi za ndani Mkoani Dodoma, na kuhakikisha wanaendelea na masomo ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Mango.

 

Pongezi hizi amezitoa hivi karibuni wakati akitoa salamu za Serikali, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa lilichofanyika katika Ukumbi wa Kepten John Komba, mjini Mbamba-bay Wilayani hapa.

 

Bi. Chilumba alimpongeza Mtendaji huyo kwa kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wameripoti Shuleni kwa asilimia mia moja, na kuanza
masomo, licha ya watoto wengine wawili, wakishirikiana na wazazi wao, ambao walipelekwa Dodoma kwa ajili ya kufanya kazi za ndani, lakini Mtendaji alihakikisha
anawachukulia hatua kali za kisheria wazazi/walezi ambao watoto wao walikuwa wakitumikishwa kwa kazi za ndani, Hivyo wanafunzi hao wamerudishwa, wako shuleni na wanaendelea na masomo.

 

“Nichukue Fursa hii kumpongeza sana Afisa Mtendaji Kata ya Kihagara na Kamati nzima ya Maendeleo ya Kata ya Kihagara, kwa kuwarudisha wanafunzi wawili waliokuwa
wakitumikishwa kazi za ndani Mkoani Dodoma, kwa kuwarudisha na kwa sasa wanaendelea na masomo, katika shule ya Sekondari ya Mango Wilayani hapa. Nahitaji
Watendaji wote muige Mfano wa Mtendaji wa Kihagara.

 

Kama ameweza kuwatoa watoto Dodoma na kuwarudisha shule wewe, wanafunzi unao katika eneo lako la utawala kwa nini Wasiende shule? Nahitaji wanafunzi wote waripoti kwa asilimia mia moja ifikapo Februari 29 mwaka huu. Alisema Chilumba.

 

Aidha aliwaagiza madiwani na Watendaji wa Kata kuhakikisha wanasaidiana na wakuu wa shule, kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea katika shule hizo kwa kuwa mwaka huu ,kuna changamoto chanya ya kupokea wanafunzi wengi zaidi kuliko miaka iliyopita.Hivyo changamoto ya Madarasa na meza zitatuliwe mapema kama walivyoanza kutatua changamoto hizo.

 

Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Kihagara alitaja mbinu alizotumia ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti ni, kutoa Elimu kwa wazazi/ walezi na watoto, tangu wanapomaliza elimu ya Msingi kwa kuwaambia kuwa bado ni wanafunzi na hawaruhusiwi kufanya chochote isipokuwa ni kujiandaa na kuendelea na masomo ya
Sekondari, hali inayowafanya wahitimu hao kusubiri kwenda shule. Njia nyingine ni kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi wasiowapeleka shule watoto wao.

 

Aliongeza kuwa Ushirikiano anaopata kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Kihagara, Mh George Ndimbo na wajumbe wake na Viongozi wa Vijiji ndio unaompelekea kufanikisha Malengo yake aliyojiwekea.

 

Mh.Mkuu wa Wilaya ya Nyasa akitoa hali ya Uripoti wa wanafunzi wa Sekondari alisema mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 2813 ambao ni sawa na asilimia tisini (90%)
wameanza masomo katika shule zote za Serikali na akawaagiza Maafisa watendaji kata wote kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka huu 2020 wanaripoti kwa asilimia (100%).