************************
Na Magreth Mbinga
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda amesema hakuna mtoto atakaekosa kwenda shule kwasababu ya upungufu wa madarasa.
Makonda amesema hayo katika kikao Cha kamati ya ushauri mkoa na kuongeza kuwa ufaulu umeongezeka kwa kiwango kikubwa katika mkoa wa Dar es Salaam.
“Serikali imetenga bajeti ya billioni 640 kwa mwaka 2019-2020 na makadirio ya billioni 685 kwa mwaka 2020-2021”.amesema Makonda
Pia Makonda amesema katika kiasi hicho cha pesa ya maendeleo billioni 1 imetengwa kwa ajili ya maboresho ya utoaji elimu bure katika mkoa wa Dar es Salaam.
Vilevile amesema katika wilaya zote wilaya hizo zimeongeza vituo vya afya,ofisi na nyumba za madaktari na hospitali za wilaya na mradi wa jengo la bima ya afya linalojengwa wilaya ya kinondoni pamoja na ujenzi wa hospitali ya Kawe na Bunju A ili wasaidie kupunguza msongamano katika hospitali ya Mwananyamala.
Makonda pia amewapongeza wananchi wa jiji la Dar es Salaam kwa kuitikia zoezi la kuhuisha taarifa zao katika daftari la mpiga kura ambayo inawapa uhalali wa kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika hapo baadae nchini