**************************
HII NDIYO TAMISEMI YA WANANCHI
Ofisi ya Rais TAMISEMI imejidhihirisha kwamba ni Ofisi ya wananchi kwa kuamua kufanya mambo magumu ambayo kwa jicho la kawaida unaweza kusema hayawezekani.
Hii imejidhirisha baada ya Waziri anaye ongoza wizara hiyo kuwapongeza watu wake kwa kufanikisha ujenzi wa majengo mawili ya Kisasa katika Mji wa Serikali.
Majengo hayo ni jengo la Ofisi kuu ya TAMISEMI na jengo la Makao Makuu ya TARURA.
Majengo hayo ambayo yamejengwa kwa maelekezo na usimamizi wa Waziri Jafo yamekuwa ni kivutio kikubwa katika Mji wa Serikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Majengo hayo yamejengwa kwa mtindo wa Ki-TAMISEMI yaani “Force Account” ni fundisho kwa Mikoa, Wilaya, na halmashauri zote nchini juu ya umuhimu wa kujali thamani ya fedha(value for money).
Hii imethihirisha usemi wa “TAMISEMI ya wananchi”