********************************
Na Silvia Mchuruza,
Bukoba.
Chama cha wanawake wajasiliamali Tanzania kimetoa mafunzo mkoani kagera kuhusu kanuni,taratibu na sheria za biashara ya mpakani kwa wanawake wajasiliamali kutoka wilaya zote za mkoa wa kagera.
Akizungumza na wajasiliamali hao katika mafunzo hayo yaliyofanyika ukumbi wa ELCT BUKOBA Kaimu Mkurugenzi wa TWCC Bi.Mwajuma Hamza ambapo amesema kuwa wataweza kuwafundisha wanawake kuchangamka fursa za kibiashara mipakani na hata jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na mkoa wa kagera kupakana na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki na kuwawezesha kujua soko kubwa la bidhaa zao walizo nazo.
“Tunataka kuwafanya wanawake wajue mfumo wetu mpya tulio uanzisha ambapo mwanamke ataweza kuripoti tatizo lake popote pale alipo hasa akiwa mpakani na changamoto kubwa atakayokutana nayo kupitia mfumo huu ili kuwawezesha kufanya biashara kuweza kuendeleza familia zao na kujiinua kiuchumi”
Hata hivyo ameongeza kwa kusema kuwa katika mafunzo hayo yatawashirikisha watu kutoka idara mbali mbali kama uhamiaji,TRA,na hata TBS na mamlaka nyingine tofauti.
Nae afisa biashara wa mkoa kagera Bw. Isaya Tendega ambae pia alikaimu nafasi ya mgeni rasimi katibu tawala wa mkoa kagera amesema kuwa Tanzania imepakana na nchi takribani nne ambapo itawasaidia wafanyabiashara wanawake kufanya biashara hata nje ya nchi au Afrika Mashariki kwa ujumla.
Hata hivyo ameongeza kwa kusema mkoa wa kagera umeanzisha madawati ya kuwatetea wanawake katika biashara hivyo wanatakiwa kufanya biashara kwa nguvu zao zote na hata wale wanaotoa biashara mipakani na kikubwa katika hayo ni kufuata taratibu.
“Mkoa wa kagera umezungukwa na fursa nyingi sana tukishirikia tunaweza kupeleka hata bidhaa zetu tunazotengeneza kwa mikono yetu lakini yote haya ili yawepo tunatakiwa kufuata taratibu na kushauriana kutafuta masoko bora”
Hata hivyo pia ameongeza kwa kusema kuwa kila biashara ina changamoto zake na changamoto zilipo ni uzalishaji hafifu na uzalishaji mdogo ili kukabiliana na changamoto hizo wanawake wanatakiwa kushirikiana katika biashara ili kupata masoko yaliyo makubwa zaidi.
Aidha nae mkurugenzi wa TWCC ambae pia ni mwenyekiti wa wanachama TWCC Bi. Mwajuma Ankon amewataka wanawake kufanya biashara inayotambulika na serikali na kuweza kurasimisha biashara zao katika mamlaka husika wapofanya biashara zao mpakani.
Vilevile nae Bi.Jovitha Juston kutoka wilaya ya Muleba ambae alikuwa mmoja wa washiriki amesema mafunzo hayo yatawasaidia katika kuelewa ufanyaji wa biashara ya mipakani ambapo pia kupitia mafunzo hayo wataweza kuyajua masoko ya ndani na nje ya nchi au Afrika Mashariki.