Home Biashara KILIMANJARO MARATHON YAWAONYA WADANGANYIFU

KILIMANJARO MARATHON YAWAONYA WADANGANYIFU

0

 Wakazi wa Dar es Salaam wakichukua namba za kukimbilia kwa ajili yam bio za KM 42 za Kilimanjaro Premium Lager na Km 21 za Tigo na kujiandikisha kwa mbio za Km 5 za Grand Malt katika viwanja vya Mlimani City mwishoni mwa wiki. Zoezi hilo litahamia Arusha kesho Jumanne na Jumatano.

 

 

 

 

 

 Waandaaji wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2020 wametoa onyo kalikwa washiriki wanaopanga kutumia njia za udanganyifu kushiriki mbio hizo kwa lengo la kujipatia medali na zawadi nyingine.

 
Taarifa iliyotolewa na waandaaji hao ilisema watu wa aina hiyo wamekuwa wakijitokeza kila mwaka huku wakitaka kushiriki kwa kutumia namba bandia. 
Mkurugenzi wa mbio hizo kitaifa, John Bayo alisema safari hii watashirikiana na jeshi la polisi na walinzikutoka kampuni ya Garda World kuwaondoa wadanganyifu hao na kuwashitaki ili sharia ichukue mkondo wake.
 
“Tunatoa onyo kali kwa wote wenye nia ya kutumia udanganyifu kwani hili ni kosa kubwa na tutawshitaki,” akisema na kutolea mfano wa wale ambao wanatumia namba za km 5 kumimbia mbio za Kilimanjaro Premium Lager KM 42 au za Tigo Km 21.
 
Alisema wengi hudanganya katika mbio hizi mbili kwa sababu zina medali na zawadi za fedha taslimu.
 
“Washiriki wote wanatakiwa kutambua kuwa tuna mtambo wa kisasa kabisa unaotunza muda na kumfuatilia kila mshiriki ambao unawezeshwa na mtandao wa Tigo wa 4G kwa hivyo tuna uwezo wa kuwanasa wadanganyifu wote kwa hivyo tunawaonya kwa sababu safari hii hatutawaachia bure tutawachukulia hatua za kisheria.
 
Katika hatua nyingine, zoezi la utoaji namba za kukimbilia kwa mbio za Km 42 na 21 lilianza kwa kasi ikiwemo pia kujiandikisha kwa mbio za km 5.
 
Baada ya hapo zoezi hilo litahamia Arusha kesho Jumanne na Jumatano katika hoteli ya Kibo Palace kuanzia saa nane mchana hadi saa mbili usiku na baadaye Moshi Februari 27 kuania saa sita mchana hadi saa kumi na moja jioni, Februari 28 saa nne asubuhi hadi saa mbili mchana na Februari 29 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni  baada ya hapo zoezi zima litasitishwa tayari kwa mashindano.
 
Wadhamini wa mwaka huu ni  Kilimanjaro Premium Lager-42km, TIGO 21km, Grand Malt-5km, Kilimanjaro Water, TPC Limited, Simba Cement, Unilever, Absa Bank Tanzania Limited na watoa huduma rasmi ni Kibo Palace Hotel, Keys Hotel, GardaWorld Security, Precision Air na CMC Automobiles.
 
Mbio hizo zitanfanyika Machi 1, katika Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.