Home Michezo MESSI APIGA NNE BARCELONA YAICHAPA 5-0 EIBAR LA LIGA

MESSI APIGA NNE BARCELONA YAICHAPA 5-0 EIBAR LA LIGA

0

Lionel Messi akishangila kibabe baada ya kufunga mabao manne dakika za 14, 37, 40 na 87 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Eibar kwenye mchezo wa La Liga leo Uwanja wa Camp Nou, bao lingine likifungwa Arthur dakika ya 89. Kwa ushindi huo, kikosi cha Quique Setien kinafikisha pointi 55 katika mchezo wa 23 na kurejea kileleni mwa La Liga, sasa kikiwazidi pointi mbili mahasimu, Real Madrid ambao usiku huu wanacheza mechi yao ya 23 pia dhidi ya Levante PICHA ZAIDI SOMA HAPA