Home Mchanganyiko MGEJA:MILA NA DESTURI ZINAZOGANDAMIZA HAKI ZA MWANAMKE ZIACHWE MARA MOJA

MGEJA:MILA NA DESTURI ZINAZOGANDAMIZA HAKI ZA MWANAMKE ZIACHWE MARA MOJA

0

………………………………………………………………………………………………….

Na.Mwaandishi Wetu

Katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani,Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation Bw.Hamis Mgeja ameiasa jamii kuendelea kupinga mila na Desturi zinazomgandamiza   mwanamke kwani ana mchango mkubwa katika Jamii.

Mgeja ambaye pia ni mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Mapinduzi [CCM]mkoani Shinyanga  amesema hayo leo Februari 22,2020 wakati akizungumza na  Mtandao huu ambapo amesema kuwa Mwanamke ana nafasi kubwa za kuleta Maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na Elimu,Kiuchumi na uongozi.

Hivyo,Mgeja amesema mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati za kuwadharau  wanawake ni unyanyapaa na kufafanua kuwa katika dunia ya sasa inahitaji ushirikishwaji wa kuwapa kipaumbele wanawake katika harakati mbalimbali za Maendeleo

Aidha,Bw.Mgeja amesema wao kama Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foudation wanaipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kuweka msukumo mkubwa wa elimu pamoja na kutoa nafasi mbalimbali kwa wanawake.

Katika hatua nyingine Bw.Mgeja amewataka vijana kuacha kubweteka na badala yake wajikite katika shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato ikiwa ni pamoja na kilimo ili kutekeleza kaulimbiu ya serikali ya awamu ya Tano ya Hapa Kazi tu.

Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation inajishughulisha masuala ya Utetezi wa Haki,Utawala Bora na  kudumisha utamaduni hapa nchini.