Baadhi ya washiriki wa mafunzo na maelekezo kuhusiana na uendeshaji wa klabu za maadili kwa walimu wa shule za msingi ,sekondari na vyuo wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (hayupo katika picha) wakati akifungua mafunzo hayo leo.
Kaimu Mkuu wa Kanda ya Magharibi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Gerald Mwaitebele akitoa ufafanuzi leo wakati mafunzo na maelekezo kuhusiana na uendeshaji wa klabu za maadili kwa walimu wa shule za msingi ,sekondari na vyuo
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akifungua leo mafunzo na maelekezo kuhusiana na uendeshaji wa klabu za maadili kwa walimu wa shule za msingi ,sekondari na vyuo
Baadhi ya walimu wa Shule za Msingi katika Manispaa ya Tabora wanaoshiriki mafunzo na maelekezo kuhusiana na uendeshaji wa klabu za maadili kwa walimu wa shule za msingi ,sekondari na vyuo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi mara baada ya kufunguliwa leo.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu na Kaimu Mkuu wa Kanda ya Magharibi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Gerald Mwaitebele wakibadilishana mawazo leo wakati wa ufunguzi mafunzo na maelekezo kuhusiana na uendeshaji wa klabu za maadili kwa walimu wa shule za msingi ,sekondari na vyuo
Picha na Tiganya Vincent
………………………………………………………………………………………………………….
NA TIGANYA VINCENT
WALIMU Mkoani Tabora wametakiwa kuwalea kimaadili wanafunzi na wanavyuo ili waweze kukua katika uadilifu na uzalendo ambao utakaowawezesha kushiriki ujenzi wa Tanzania mpya msingi mkuu ni viwanda.
Kauli hiyo imetolewa leo na katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa ufunguzi wa mafunzo na maelekezo kuhusiana na uendeshaji wa klabu za maadili kwa walimu wa shule za msingi ,sekondari na vyuo.
Alisema kuwa katika kukuza uchumi Tanzania mpya ipo haja ya kuwa na vijana ambao wamekuzwa katika msingi ya uadilifu na uzalendo ambao utaweka mbele maslahi ya Taifa na sio masalahi binafisi.
“Maslahi ya Taifa yatadumu daima …lakini maslahi ya mtu binafsi ni ya muda baada ya kufa basi nayo yamekwisha” alisema.
Makungu alisema mafunzo hayo ni muhimu sana katika kujenga jamii yenye maadili mema ambayo yatasaidia kuzalisha Viongozi wazalenda na waadilifu.
Aidha Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwapongeza walimu kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya kukuza maadili mkoani Tabora na kuongeza kuwa uanzishwaji wa Klabu za Maadili utaleta mabadiliko chanya na kuongeza ufaulu kwa vijana mashuleni na vyuoni.
Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Kanda ya Magharibi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Gerald Mwaitebele alisema Ofisi hiyo imeamua kuanzishia Klabu hizo ili kuwajenga vijana tangu awali ili kuwajenga kukua kimaadili na uzalendo wakiwa wadogo.
Alisema ni kazi kubwa kufundisha umuhimu wa maadili kwa mtu mzima kuliko kufundisha akiwa mdogo kwa kuwa atajengeka katika hali ya uadilifu na kuipenda nchi yake.
Mafunzo hayo ya siku moja yameshirikisha walimu wa shule za Msingi, sekondari na Vyuo vya Elimu vilivyopo Manispaa ya Tabora na yalikuwa na mada za Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Mgongano wa Masilahi na Mwongozo wa Uanzishwaji na Uendeshaji wa Klabu za Maadili