Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, BI. Devota Mdachi akimkabidhi bendera mrembo Graatness A. Nkuba katika ofisi za TTB jijini Dar es salaam.
Katika picha ya pamoja, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, BI. Devota Mdachi (Kushoto) akiwa na mrembo Graatness Nkuba pamoja na Meneja wake Miriam Ikoa.
Mrembo Graatness Nkuba akionyesha baadhi ya vipeperushi akivykabidhiwa na Bodi ya Utalii Tanzania.
……………………………………………………………………………………………………..
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeendelea kutumia fursa ya mashindano ya urembo ya kimataifa kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania. Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi Devota Mdachi amemkabidhi mrembo Graatness Nkuba bendera na vipeperushi vyenye taarifa za utalii wa Tanzania kabla ya kuanza safari yake ya kwenda kushiriki shindano la urembo nchini Vietmnam.
Mlimbwende Greatness ni Mtanzania pekee anayetarajia kuiwakilisha Tanzania katika shindano la “Miss Charm International” ambalo linalenga kumtafuta mrembo mwenye haiba, mvuto na ambaye atabeba utamaduni, elimu na kuutangaza utalii wa nchi yake. Shindano hili litahusisha warembo kutoka nchi 50, linatarajia kufanyika katika mji wa Ho Chi Minh nchini Vietman kuanzia tarehe 5 – 17 mwezi machi, 2020.
Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika Februari 21, 2020 katika ofisi ya TTB iliyopo jijini Dar es salaam, Bi. Devota alisema “Tunakukabidhi vipeperushi ambavyo ni nyezo utakayoitumia kuwahamasisha na kuwavutia warembo wengine waje kuvitembelea na kujionea utajiri wa vivutio vya asili vilivyopo katika nchi ya Tanzania pamoja na kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano hayo ili dunia itambuwe kuwa “Tanzania Unforgettable”.
Tanzania kuwa na mwakilishi katika mashindano haya kutasaidia kulifungua soko la utalii la nchi ya Vietnam.