|
Mbunge wa Jimbo la Lupembe, Joramu Hongoli akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Lupembe, mkoani Njombe, ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuimarisha umoja na mshikamano kati ya wananchi na viongozi mbalimbali ili kurahisisisha kutatua kero na kuleta maendeleo katika Kata hiyo. Pia alizungumzia suluhisho la malipo ya wakulima wa chai wanaovidai viwanda . Aliwatoa hofu kwamba wasiwe na wasiwasi serikali iko pamoja nao na kwamba fedha zao watalipwa hivi punde. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Lupembe (VEO) wa Lupembe, Mary Ngumbi, Katibu Kata wa CCM Lupembe, Lawrent Mangula na Diwani wa Kata ya Lupembe, Laiton Mbuna. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA |
|
Mmoja wa wazee wa Kijiji cha Lupembe, akisikiliza kwa makini wakati Mbunge wao, Hongoli akihutubia na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayotendeka jimboni humo. |
Baadhi ya akina mama wakiwa katika mkutano huo.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo uliokuwa ukihutubiwa na Mbunge wa Jimbo la Lupembe, Joramu Hongoli.
Mbunge Hongoli akisisiza jambo wakati wa mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Lupembe (OCS), Christopher, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Lupembe (WEO), Hilda Nyitike na Sheddy Malekela ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Lupembe.