Home Siasa TUPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA NCHINI-NCCR MAGEUZI

TUPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA NCHINI-NCCR MAGEUZI

0

 

………………………………………………………………………………………….

Na Magreth Mbinga

NCCR MAGEUZI ipo tayari kushirikiana na chama chochote cha siasa kwaajili ya kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo endapo watafikia makubaliano na chama hicho.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia leo kwenye mkutano na waandishi wa habari Jijin Dar es salaam.

Mbatia amesema kuwa watashiriki kikamilifu kwenye uchaguzi Mkuu mwaka huu katika ngazi zote kuanzia udiwani,ubunge,Uraisi kwa upande wa Tanzania bara na Baraza la wawakilishi na Uraisi kwa upande wa Tanzania visiwani.

Vilevile watashirikiana na watu mbalimbali kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa mwaka huu ili mfumo wa vyama vingi uendelee hata Mara baada ya Uchaguzi Mkuu kupita.

“Tutatumia mfumo wetu wa ndani ya Chama ili kushawishi wananchi kujiunga na chama chetu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama”.Alisema Mbatia

Hata hivyo viongozi wametakiwa wawaenzi waasisi wa muungano kwa kuwahamasisha wananchi kupiga kura.