Home Mchanganyiko NBC YAFANIKIWA KUTOA HUDHUMA ZA MATIBABU BILA MALIPO KWA WATU MILIONI 3.3

NBC YAFANIKIWA KUTOA HUDHUMA ZA MATIBABU BILA MALIPO KWA WATU MILIONI 3.3

0


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akisalimiana na Afisa Masoko Tawi la NBC Samora Dustane Lipawaga akiwa na Meneja Uhusiano wa Benki ya Kibiashara ya NBC William Kallaghe (kulia) na Meneja huduma za Jamii Irene Peter wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT)  yaliyofanyika leo (jana)  yakihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Benki ya Kibiashara ya NBC William Kallaghe (kulia), wengine ni Afisa Masoko Tawi la NBC Samora Dustane Lipawaga (kushoto) na Meneja huduma za Jamii Irene Peter wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yaliyofanyika leo (jana) yakihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Askofu wa Kanisa la Mennonite, Dayosisi ya Mashariki na Pwani Askofu Nelson Kisare akielezea jambo kwa kwa Meneja Uhusiano wa Benki ya Kibiashara ya NBC William Kallaghe (wa pili kulia), wengine ni Afisa Masoko Tawi la NBC Samora Dustane Lipawaga (kulia) na Meneja huduma za Jamii Irene Peter (kushoto)  wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yaliyofanyika leo (jana) yakihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli 

…………………………………………………………………………………………………………

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema kuwa jumla ya watu Milioni 3.3 wamefanikiwa [email protected] huduma za [email protected] bila malipo zinazoendeshwa na benki hiyo chini ya programu yake ya kliniki zinazohamishika iliyoanzishwa tangu mwaka 2002.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam jana na Msemaji wa NBC, William Kalaghe [email protected] akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa madaktari na Rais John Magufuli kuelekea maadhimisho ya siku ya madaktari nchini yanayodhaminiwa na benki hiyo.
Alisema wamekuwa wakitoa huduma hiyo ya bila malipo kwa kinamama na watoto chini ya umri wa miaka mitano na kuongeza kuwa [email protected] huduma hiyo kundi hilo limeweza kupata huduma na @ba za magonjwa mbalimbali.
Kalaghe alisema wanatoa huduma hiyo [email protected] kliniki zao zinazohamishika ambazo ni magari yanayopita mitaani [email protected] na kutoa huduma hiyo ya bila malipo kwa kinamama na watoto hao.
“Tumeanza programu hii tangu mwaka 2002 na mpaka sasa tuna jumla ya magari matatu ambayo yapo barabarani yakifanya huduma hiyo nayo jumla ya wagonjwa waliohudumiwa chini ya mpango huo wamefikia Milioni 3.3 ambao wengi wao ni wakazi wa Jiji la Dar es Salaam,” alisema.
Aidha alisema sababu kubwa ya yao kudhamini maadhimisho hayo ya miaka 55 ya madaktari nchini, ni kutokana na benki hiyo kuwa wadau wa sekta ya afya kwani wamekuwa wakiunga mkono sekta hiyo hususani [email protected] masuala ya huduma za mama na mtoto.
“Sababu nyingine zilizotufanya tudhamini maadhimisho haya ni umuhimu na mchango wa madaktari [email protected] Taifa letu hivyo sisi tumeona ni vema tushirikiane nao kama wadau wao, japokuwa tunatoka sekta ya kifedha tumeona lazima twende sambasamba na sekta ya afya kwani lengo letu ni moja wao wanaimarisha afya za watanzania na sisi tunahakikisha watanzania wanawezeshwa,” alisema
Hata hivyo alisema benki hiyo imekuwa ikitoa mitaji kwa hospitali binafsi ambao wanamahitaji ya kuagiza mitambo kutoka nje ya nchi kwa [email protected] mikopo.
Naye Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Elisha [email protected] alisema chama hicho [email protected] miaka 55 tangu kuanzishwa kwake na Machi 4 mwaka huu watakuwa na kambi ya utoaji wa huduma za [email protected] bila malipo [email protected] viwanja vya Zakhem Mbagala.
Alisema [email protected] chama hicho kinaanzishwa kilikuwa na madaktari 23 lakini hivi sasa wamefika zaidi ya 15,000 na kuongeza kuwa [email protected] ya hao kuna madaktari vijana ambao wapo tayari kwenda kufanya kazi mahali popote nchini.

Kuhusu Na7onal Bank of Commerce (NBC)

Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya zamani kuliko zote nchini Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha.

Benki hii inaanzia mwaka 1967 ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha taasisi zote za fedha, zikiwamo benki. Mwaka 1991, sheria ya mabenki ilirekebishwa na miaka sita baadae, yaan mwaka 1997, taasisi iliyojulikana kama Benki ya Taifa ya biashara, iligawanywa [email protected] tanzu tatu [email protected]: NBC Holding [email protected], [email protected] Microfiance Bank (NMB) na NBC (1997) Limited. Mwaka 2000, Benki ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata hisa 55% kutoka NBC (1997) Limited. Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), ilipata 15% ya hisa za benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.

Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa [email protected] [email protected] maeneo mbalimbali nchini. Ikiwa na matawi 5 na mashine za ATM zaidi ya 230, Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali za ukusanyaji fedha za huduma nyingine za kibenki kwa wateja mbalimbali. Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi takriban 1,200 nchi nzima.