Wananchi wa kata wa Mkange wakimsikilza Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu(hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhari uliyofanyika kwenye kata hiyo, iliyopo kwenye Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Mafundi wakiwa wanaendelea na kazi ya uwekaji nguzo kwenye kata ya Mkange, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akiongea na Wananchi wa kata ya Mkange kwenye mkutano wa hadhara wakati alipoenda kwenye alikuwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme kwenya kata hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu( wa kwanza kulia baada ya nguzo) akitikia dua pamoja na wananchi wa Mkange mara baada ya kuwekwa nguzo katika kata hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akiweka mchanga kwenye nguzo kuashiria kuwa umeme umefika katika kata ya Mkange,wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
*******************************
Hafsa Omar-Pwani
Wananchi wa mtaa wa Mkange uliopo katika Kata ya Mkange wilaya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wameishukuru Serikali ya Awamu ya tano kwa kuzindua rasmi kazi ya usambazaji umeme wa Mradi wa Peri-Urban kwenye maeneo ambayo sio mji au kijiji katika kata hiyo.
Tukio hilo limetokea, Februari 20,2020 katika kata hiyo,wakati Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipokuwa kwenye ziara ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini na kuzindua rasmi kazi za usambazaji umeme kwenye kata hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema kuwa,walikuwa wanasubiri kupata huduma hiyo kwa mda mrefu, lakini wanaishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwaletea umeme kwenye kata yao,na utawasaidia kwa matumizi mbalimbali hasa katika huduma za jamii ambapo walikuwa wanapata changamoto kubwa bila umeme.
Akizungumza katika Mkutano wa hadhara kwenye kata hiyo, Naibu Waziri alisema kata hiyo ni moja kati ya kata ambayo inachangia sana uchumi wa Taifa, kwasababu ndio kata inayopatikana hifadhi ya Taifa ya Sadan.
Aidha, alisema kuanza rasmi kwa usambazwaji wa umeme ambao Serikali umeugharamia kwa pesa nyingi, itakuwa fursa kwa wanakijiji hao kujikwamua kiuchumi na kuwataka wananchi wa kata hiyo kuutunza na mradi huo na wajitokeze kwa wingi kulipia 27000 ili waweze kunganishiwa na huduma hiyo.
“Nawaomba ndugu zangu tuombe mradi uende kwa wepesi na mkikubali wana Mkange mradi uende kwa wepesi utakwenda kwa wepesi, ndio tunaianza safari sasa ya kuwasha taa ya kwanza katika kata hii kubwa ya Mkange”
Vilevile, aliwataka REA, Wakala wa Nishati Vijijini kutafuta wakandarasi wenye uwezo wa kufanya kazi kwenye maeneo ambayo yenye changamoto bila ya malalamiko yoyote kwenye miradi inatakayoanza hivi karibuni.
“ Mmeona tumepita katikati ya mbuga mtakapokwenda kwenye taratibu za manunuzi msitulete wakandarasi wababaishaji tunataka wakandarasi wenye uwezo wa kuhimili maeneo kama hayo, hatutaki mkandarasi ambaye atasema mvua inanyesha gari haipitiki hii hapana”Alisema.