Home Burudani MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA KUCHANGIA MAHITAJI YA WATU WENYE UALBINO

MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA KUCHANGIA MAHITAJI YA WATU WENYE UALBINO

0

Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania kwa pamoja na Tanzania Cosmetology Association  Fashion Association of Tanzania [FAT] na Feza alumni foundation tunayo furaha kubwa
kuufahamisha umma wa watanzania kuwa tunaandaa mbio na matembezi ya hisani yatakayofanyika
siku ya jumamosi tar 07 Machi 2020 yatakayobeba jina la Abinism charity walk and run 2020. Mbio
na matembezi hayo ya kilomita tano (5) yanatarajiwa kuanza kwenye Parishi ya Mt Peter saa 12
asubuhi na kuhitimishwa saa 4 asubuhi kwenye hotel ya Sea Cliff, Masaki, Dar es Salaam.
Itakumbukwa kuwa watu wengi wenye ualbino hupoteza maisha wakiwa kwenye umri mdogo kwa
sababu ya saratani ya ngozi itokanayo na mionzi mikali ya jua, hivyo basi ili kuyaenzi na
kuyaendeleza mazuri yote ambayo yamefanywa na yanayoendelea kufanywa na Serikali yetu kwa
pamoja na wadau wa ndani na nje ya nchi, tumeona pia ni vyema kwa umoja wetu kuandaa mbio na
matembezi haya ambapo pesa itakayopatikana itatumika kununulia mafuta kinga ya ngozi pamoja
na kofia zenye kingo pana ili kupunguza changamoto ya saratani ya ngozi inayowakabili watu wenye
ualbino. 
Tunaiomba jamii ya watanzania, kimataifa, watu binafsi, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali
zikiwemo taasisi za dini tushirikiane kufanikisha matembezi haya muhimu kwa ustawi wa watu
wenye ualbino pamoja na familia zao kwa kununua t-shirt kwa gharama ya tsh 35,000/= kwa t-shirt
moja. Lakini pia siku hiyo unaweza kutuletea Mafuta kinga (sunscreen lotion SPF 30+) pamoja na
Kofia zenye kingo pana (wide brimmed hats) ikiwa ni lengo la kufanya matembezi haya.
2
Jisajili sasa Pia waweza kununua t-shirt yako
kupitia selcom Masterpass 60347937- TCA ama kupitia akaunti ya Chama cha Watu Wenye Ualbino
Tanzania iliyopo NMB bank namba 20110003046, kwa mawasiliano zaidi tupigie kupitia namba za
simu 0684 771 749 au 0767 076 226.