*********************
Tarehe 19 Februari, 2020 Serikali ya China imetoa taarifa kuhusu maelekezo na miongozo
mbali mbali kuhusiana na masuala ya kiutawala, kitaaluma na kikonseli kwa Wanafunzi wa
Kigeni (International Students) kama ifuatavyo:-
Masuala ya Kiutawala
• Idara za Elimu za Majimbo zimeelekezwa kusimamia Vyuo Vikuu katika kukabiliana na kudhibiti maambukizi ya COVID-19 kwa Wanafunzi wa Kigeni.
• Idara za Elimu za Majimbo/Jiji zimeelekeza Vyuo Vikuu kuunda timu za kutoa huduma mbali mbali zinazoendana na mipango ya udhibiti wa maambukizi ya COVID-19 kwa Wanafunzi wa Kigeni.
• Serikali ya China imeelekeza kugawa bure ‘masks, sanitizers’, vifaa mbali mbali vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa pamoja na kusimamia upatikanaji wa huduma za chakula (kwenye canteens au kwa kuagiza) kwa wanafunzi wanaoishi vyuoni.
• Kwa wanafunzi wanaoishi nje ya vyuo (off campus students), changamoto zinazojitokeza wanapaswa kuwasiliana na vyuo vyao au kamati za mitaa
(community committees) za mahali wanakoishi.
• Kuwahimiza Wanafunzi wa Kigeni hususan waliopo Jimbo la Hubei kupitia mitandao maalum iliyoandaliwa na Serikali ya China katika maeneo waliyopo kwa ajili ya kupata miongozo na huduma za ushauri nasaha.
KUAHIRISHWA KUFUNGUA VYUO VIKUU
Kufuatia uamuzi wa Serikali ya China wa kuahirishwa kufungua vyuo vikuu kwa muhula
wa 2020 (Spring Semester of 2020), wanafunzi wote wameelekezwa kuzingatia mambo
muhimu yafuatayo:-
• Muda wa kufungua Vyuo Vikuu utapangwa na Serikali za Majimbo kulingana na tathmini ya hali ya maendeleo ya ugonjwa wa COVID-19 katika maeneo yao.
• Wanafunzi wa Kigeni wafanye mawasiliano ya mara kwa mara na Vyuo Vikuu wanavyosoma ili kufahamu tarehe kamili ya kurejea vyuoni.
• Wanafunzi wa Kigeni wametakiwa kutorejea Chuoni hadi pale watakapopewa taarifa rasmi (notice) kutoka mamlaka za vyuo vyao kuhusu tarehe za kufungua chuo.
• . Baadhi ya vyuo vimeanzisha utaratibu wa muda wa kutoa mafunzo kwa njia ya
mtandao. Wanafunzi wote wanaosoma nchini China wanahimizwa kufanya
mawasiliano na vyuo vyao ili kupata taarifa kama kozi zao zitaendeshwa kwa njia
ya mtandao na muda wa kuanza masomo hayo.
KUHUSU WANAFUNZI WANAOFADHILIWA NA SERIKALI YA CHINA
(SCHOLARSHIPS)
Kwa upande wa suala la ufadhili (scholarships), Serikali ya China imeelekeza:-
• Kwa Wanafunzi wa Kigeni wenye udhamini walioondoka China, posho zao
(scholarship living allowance) zitasitishwa hadi watakaporejea vyuoni.
• Wanafunzi wa Kigeni ambao ni wapya waliopata ufadhili kwa Mwaka wa Masomo
wa 2019/2020 (Spring 2019/2020 Academic Year), wafanye mawasiliano na vyuo
vyao ili kupata mwongozo.
• Wanafunzi wa Kigeni watakaotaka kuahirisha masomo wanaweza kufanya hivyo
kwa kuwasiliana na vyuo vyao na kuwa China Scholarship Council (CSC)
itaidhinisha kuendelea kwa udhamini wao lakini kwa sharti kuahirishwa huko
kusiwe zaidi ya mwaka.
• Kwa pande wa udahili wa mwaka wa masomo wa 2020/2021, mchakato wake
unaendelea na haujakoma.
3
MASUALA YA KIKONSELI
• Wanafunzi wote wa kigeni ambao vibali vyao vya kuishi au VISA vinakaribia
kumalizika muda wake wanatakiwa kufika katika ofisi za uhamiaji kuongeza muda
wa kupata vibali na VISA mpya haraka.
• Katika kipindi chote cha mapambano dhidi ya covid-19 Ofisi za Uhamiaji zitakuwa
wazi kutoa huduma, hivyo raia wa kigeni watumie nafasi hiyo kupata huduma hizo.
Kwa watakaopata matatizo yoyote wawasiliane na ofisi za mambo ya nje (FAO) za
mahali walipo.
• Kwa wanafunzi waliopo nje ya nchi na ambao VISA au vibali vyao vya kuishi nchini
China vitakuwa vimemalizika muda wao wafike ofisi za Balozi za China katika nchi
zao kuongeza muda wa VISA zao (extension).