Home Mchanganyiko WAKULIMA KATAVI KUONDOKANA NA ADHA YA JEMBE LA MKONO

WAKULIMA KATAVI KUONDOKANA NA ADHA YA JEMBE LA MKONO

0

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga akikata utepe katika Trekta kabla ya kumkabidhi mkulima Gabriel Kinyonto.

Trekta lililokabidhiwa kwa mkulima.

******************************

Na mwandishi wetu

Baadhi ya wakulima mkoani katavi wameondokana na adha ya kilimo cha jembe la mkono baada ya kupata mikopo ya zana za kilimo hali inayotarajiwa kuinua uchumi wa kaya na mkoa kwa ujumla

Hii inatokana na kupata mikopo ya zana za kilimo

Akikabidhi trekta kwa mmoja wa wakulima kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa katavi; mkuu wa wilaya ya mpanda Lilian Matinga amewataka wakulima kuachana na kilimo cha kizamani

Wakizungumza mara baada ya kupokea trekta hilo; ambalo ni mkopo wa shilingi milioni thelathini kutoka benki ya crdb; wakulima hao wamesema trekta hilo litawasaidia katika kutimiza malengo yao

 

Kwa upande waoMeneja wa CRDB tawi la Mpanda bwana Hamad Masoud ametoa wito kwa wakulima kufika katika benki hiyo kwa ajili ya kuomba mikopo ya zana za kilimo ili kujiendeleza

Naye Mhandisi Wilson Godfrey kutoka kampuni ETC amabo ni wauzaji wa matrekta hayo amesema wakulima wanahitaji kubadilika kwa kuboresha zana za kilimo ili kuendana na mabadiliko kwani Tanzanzia ya sasa ni ya viwanda