***************************
MWANZA.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Mwita Waitara amewataka wafanyabiashara Jijini Mwanza kujiunga kwenye vikundi ili wapewe mkopo wa halmashauri usio na riba utakaoweza kuwasaidia katika shughuli zao za kibiashara.
Ameyasema hayo baada ya kuwatembelea wamachinga wa soko la Makoroboi Jijini Mwanza baada ya kuungua kwa soko hilo hivi karibuni na kusababisha hasara za mali zao.
Aidha, Mhe.Waitara amewataka viongozi wa wafanyabiashara kote nchini kushirikiana na jeshi la zimamoto ili kupata elimu ya namna ya kukabiliana na majanga yatokanayo na moto
Nae Mwenyekiti wa Machinga taifa Bw.Ernest Matondo ameiomba serikali kutoa msaada wa haraka kwa wafanyabiashara ambao wamepatwa na janga hilo.
Wakiwa katika eneo hilo wafanyabiashara wa eneo hilo wamesema kuwa hasara hiyo imepelekea kushindwa kumudu hali ya maisha na kushindwa kuchangia pato la nchini kwa kulipa ushuru.