Home Mchanganyiko MAVUNDE ASAFISHA NJIA MWEZI OKTOBA,2020

MAVUNDE ASAFISHA NJIA MWEZI OKTOBA,2020

0

 Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde,akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo kabla ya kuzindua  shule shikizi ya Msingi  Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma.

Wanafunzi wa shule ya shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma wakitoa burudani kwa mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo kabla ya kuzindua  shule hiyo. 

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde,akiwa na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo ,wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Glaring Future Foundation(GFF), Bi. Aisha Msantu wakati wa uzinduzi shule ya shikizi ya msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi,akizungumza kabla ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo  kuzindua  shule shikizi ya Msingi  Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma.

Meya wa Jiji la Dodoma, Prof David Mwamfupe,akizungumza kabla ya uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo aliyefanikisha ujenzi huo ni Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi,akizungumza kwenye uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo aliyefanikisha ujenzi huo ni Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Binilith Mahenge,,akizungumza kwenye uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo aliyefanikisha ujenzi huo ni Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, vijana na Ajira,ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde,akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni yeye Mhe.Mbunge.

Sehemu ya wanafunzi wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, vijana na Ajira,ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde,alipokuwa akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni yeye Mhe.Mbunge.

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, vijana na Ajira,ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde,akisisitiza jambo kwa  wananchi katika uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni yeye Mhe.Mbunge,kulia ni Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akizungumza kwenye  uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde.

Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Chiwondo wakifatilia uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma.

Muonekano wa jengo la darasa lililozinduliwa katika  shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde ndiye aliyefanikisha ujenzi wa shule hii.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akizindua rasmi  shule shikizi ya msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde.

Na.Alex Sonna-Fullshangweblog

……………………………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde amesema kufikia 2021 shule zote za msingi sitakuwa zimepatiwa umeme ili kuweza kutumia kompyuta katika kuboresha sekta ya elimu kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya tano.

Kauli hiyo ameitoa leo  katika Uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyojengwa  kwa msaada wake akishirikiana na Halmashauri ya Jiji hilo ambapo tayari vyumba vinne vya madarasa vimeshakamilika huku vingine vitatu vikiwa kwenye ujenzi.

Mhe. Mavunde amesema serikali imetenga billion 50 ili kuweza kukamilisha usambazaji wa umeme katika maeneo yaliyobaki bila kupatiwa umeme.

“Kwa shule zilobaki bila kupatiwa umeme nitahakikisha kabla ya mwaka huu 2020 haujaisha wanapatiwa umeme ili pia waweze kupatiwa kompyuta zitakazo wafanya kunufaika na elimu bora wanayotakiwa kupata watoto wetu wa kitanzania”amesema Mavunde

Mavunde amesema kuwa pia uchimbaji wa visima vya maji 13 unaendelea na katika visima hivyo kata ya Nala nao ni miongoni mwa wanufahika wa visima hivyo lengo likiwa ni kuwapatia wananchi wake huduma ya maji.

Akizungumza mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa anatambua juhudi za TAMISEMI katika sekta ya elimu hivyo anaunga mkono juhudi hizo kwa kukarabati miundombinu ya elimu ili kuhakikisha elimu bora inapatikana kwa kila mtanzania.

Lakini Pia amewataka wananchi wa kata hiyo kutunza miundo mbinu na kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha Watoto wao wanapata elimu ili waje kulitumikia taifa lao wakati ukifika.

Mavunde amesema  kuwa ujenzi wa shule hiyo utasaidia kupunguza kero kwa Watoto na wananchi wa kata hiyo kwani awali walitembea mwendo mrefu wa kilomita 20 kwenda shuleni.

Kwa upande wake Waziri Jafo amemwagiza Mkurugenzi wa Elimu TAMISEMI , Bw.Julius Nestory kabla ya mwezi wa sita mwaka huu kuwa amepeleka fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa  ili ifikapo mwakani 2021 wanafunzi wote kuwa wameacha kutembea umbali wa mwendo mrefu kufata elimu.

“Mkurugenzi wa Elimu TAMISEMI hakikisha katika ajira zitakazo toka shule hii inapewa kipaumbele cha kupatiwa walimu kwani mwakani wanafunzi wote wanaotembea mwendo mrefu kufata elimu wawe wamehamia katika shule hii ya Chiwondo.

Awali Mkurugenzi wa jiji la Dodoma  Godwini Kunambi amesema kuwa ametoa pikipiki mbili kwa walimu wa wili wanao hudumu katika shule hiyo huku akiweka wazi kuwa ofisi yake inaweka utaratibu  mzuri wa kuweza kuwajengea nyumba za kuishi walimu hao na kuepuka adha ya kutembea mwendo mrefu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Binilith Mahenge ametoa wito kwa wazazi na walezi wa wanafunzi kutoa ushirikiano kwa kuhakikisha wanafunzi wanafika shuleni na kuendelea kuchangia katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo.

Pia mdau wa maendeleo Mkurugenzi Mtendaji wa Glaring Future Foundation(GFF), Bi. Aisha Msantu,amesema  katika uzinduzi huo amechangia madawati 60 na kutoa wito kwa wananchi kuchangia miundombinu ya shule ili Watoto waweze kupata elimu bora katika mazingira sahihi.