…………………………………………………………………………………………………………
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
CHAMA Cha Ushirika Wa Wakulima Wa Umwagiliaji -Ruvu,Chalinze mkoani Pwani (CHAURU), kinadai baadhi ya wanachama wake kiasi cha sh.milioni 153 ,madeni yanayochangia kushuka kwa mapato.
Kutokana na deni hilo, ushirika huo umeagiza kila mwanachama anaedaiwa ahakikishe analipa deni lake, hadi ifikapo Novemba mwaka huu.
Akizungumzia matokeo ya ukaguzi na mapato na matumizi wakati wa mkutano mkuu wa ushirika huo ,mwenyekiti wa CHAURU ,Sadala Chacha alisema ,wadaiwa walikopa pembejeo, zana na huduma mbalimbali za kilimo.
Hata hivyo ,aliongeza kwamba malipo ya fedha hiyo itawezesha kuboresha miundombinu iliyopo.
Aidha alieleza ,mapato kijumla yameongezeka kutoka milioni 450,799,9 kwa ukaguzi wa mwaka 2017/2018 ukilinganisha na 2016/2017 ambapo walikusanya milioni 361,759,8 .
Chacha alisema ,fedha hizo ni zilitokana michango ya kilimo,kukodisha zana,michango ya kuchimba mifereji ,kuchangia mpunga,shamba na viwanja.
Pamoja na hilo, aliwaasa wakulima hao kutumia mawe yaliyopimwa na wakala wa vipimo badala ya kutumia mawe wamayotembea nayo wanunuzi wasio waaminifu na kusababisha kuibiwa na kujikuta wakipata hasara.
“Sasa changamoto imekuja kwa wakulima wasiotaka kuuza mchele wanauza mpunga kama zamani ,wanakuja hapa na wanunuzi wao ,hao wafanyabiashara wanatembea na mawe yao ambayo ni udanganyifu mtupu, wakitumia mawe hayo wanaibia wakulima kilo 17 sasa wakulima wanapata hasara kubwa”alifafanua Chacha.
Nae mkaguzi wa hesabu kutoka shirika la ukaguzi na usimamizi wa vyama vya ushirika (COASCO) ,Brighton Mwang’onda aliitaka bodi na menejiment kufanyia kazi hoja za nyuma na kutilia maanani maagizo yaliyotolewa miaka ya nyuma ili kuondoa changamoto ndogondogo zinazojitokeza wakati wa uchaguzi.
Kwa upande wa mwanachama wa CHAURU , Dando Suleiman aliomba wasimamizi wa mizani wachukuliwe hatua kwani haiwezekani kuwepo na wizi kwa wanunuzi angali wao wakiwepo bila kusimamia wakulima.