
akiangalia hatua za uchakataji wa dhahabu kwa wachimbaji wadogo kijiji cha Sambaru
wilayani Ikungi mkoani Singida ambapo aliwapa elimu kuhusu namna ya kujikinga na
wanapotumia kemikali ya zebakia ambayo ina madhara kwa afya na mazingira.

akizungumza na wachimbaji wadogo katika mgodi mdogo ulipo kijiji cha Sambaru
wilayani Manyoni mkoani Singida ambapo aliwaelimusha kuhusu madhara ya kutumia
zebaki. Kulia ni Kaimu Meneja wa Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida, Chone malebo.

akipewa maelezo kuhusu namna hatua za uchimbaji hadi uchakataji wa dhahabu
unavyofanyika wakati akiwa katika ziara eneo la wachimbaji wadogo kijiji cha Sambaru
wilayani Ikungi mkoani Singida.

akielekea kukagua shughuli wanazofanya wachimbaji wadogo pamoja na namna
wanavyotunza mazingira katika machimbo ya kijiji cha Sambaru. Kulia kwake ni Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogoro.

akiangalia namna ambavyo uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia zebaki katika mgodi
mdogo uliopo kijiji cha Sambaru wilayani Manyoni mkoani Singida ambao unafanyika
bila kutumia vifaa maalumu vya kujikinga mikono jambo ambalo linaleta madhara kwa
afya na mazingira.

alipofanya ziara ya kukagua shughuli za wachimbaji wadogo wakimsikiliza Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (hayupo pichani)
wakati akizungumza nao kuhusu madhara ya zebaki kwa afya na mazingira.

akiangalia namna ambavyo uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia zebaki katika mgodi
mdogo uliopo kijiji cha Sambaru wilayani Manyoni mkoani Singida.

akizungumza na mwananchi aliyemkuta akifanya shughuli za kuponda mawe katika eneo
la wachimbaji wadogo kijiji cha Sambaru wilayani Ikungi mkoani Singida alipofanya ziara
ya kukagua shughuli za wachimbaji wadogo.
…………………………………………………..
Na Robert Hokororo, Singida
Wakati Serikali inaendelea kuweka utaratibu wa kupata mbadala wa matumizi ya
zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu imeshauri watumie vifaa
vinavyowakinga wakati wakifanya shughuli hizo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Mussa Sima wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwa
nyakati tofauti katika vijiji vya Sambaru wilayani Ikungi na Londoni wilayani
Manyoni mkoani Singida.
Sima alisema kuwa Serikali inaendelea na kuwapa elimu wachimbaji hao katika
maeneo mbalimbali nchini ili waweze kuepuka madhara ya kiafya yanayotokana
na kemikali hiyo.
“Tanzania tuliridhia Mkataba wa Minamata mwaka jana unaotaka kupunguza
ama kuondoa kabisa matumizi ya zebaki kwa ninyi wachimbaji ili kuwaepusha
madhara ya kiafya na kimazingira katika maeneo yenu,” alisema naibu waziri.
Akiwa katika ziara hiyo ambapo alitembela kuona shughuli za uchimbaji na
kukagua namna wanavyotunza mazingira, Sima alisema kuwa jukumu la Serikali
ni kutoa elimu juu ya madhara ya zebaki ili kulinda afya za wachimbaji wadogo.
“Niwaahidi tu tutashirikiana na Ofisi ya Madini ili muweze kupata vifaa maalumu
vya kujikinga wakati wa kuchenjua badala ya mikono, tutawaletea gloves mvae
mikononi na musk wakati tunachoma ili kufunika pua kwani kemikali hii ina
madhara kiafya,” alisema.
Aidha, Naibu waziri aliwataka wachimbaji hao kuacha kukata miti wakati wa
shughuli za uchimbaji wa dhahabu na badala yake wawe na utamaduni wa
kutumia njia mbadala kama ambavyo wanavyoelekezwa na mamlaka
zinazohusika.
Aliongeza kuwa jukumu la Ofisi ya Makamu wa Rais na Serikali kwa ujumla ni
kuhakikisha nchi inakabiliana na changamoto ya mabadilkko ya tabianchi na
hivyo kuleta athari.
Alisema tunapoendelea kuchoma na kukata miti ovyo, kulima kholela na
kuchimba mashimo ovyo kwa ajili ya madini ni mambo yanayosababisha mvua
isije kwa wakati pamoja na jua kuwa kali kuliko kawaida.