Home Siasa MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM AHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA...

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM AHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA

0
meneja wa Tanroad mkoa Wa Arusha muhandisi John Kalipale akitoa maelezo kwa Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi Taifa juu ya ujenzi wa barabara ya baipass ,ambapo alisema barabara hiyo itasaidia kupunguza msongamano na foleni mjini.
Mwenyekiti Wa wazazi Taifa ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu Edmund Mundolwa akipeana mkono na Mwenyekiti Wa wazazi Ccm Taifa Herzon mbise Mara baada ya kupandisha moja ya mizinga ya Nyuki katika Kijiji cha Sakila chini ndani ya kata ya Kikatiti iliotolewa na Mwenyekiti Hugo Wa mkoa Wa Arusha kwa ajili ya wilaya ya Arumeru
Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Arusha mjini Ally Meku  akibadilishana mawazo na Katibu Wa itikadi na uwenezi wilaya ya Meru Mungure (Mwarabu) Wa pili kushoto pamoja na mbaraza Wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha  victa mollel wakati walipokuwa kwenye ziara ya Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi CCM Taifa katika ziara yake ya kutembelea wilaya zote za mkoa Wa Arusha(Picha zote na Woinde Shizza,Arusha).

…………………………………………………………

Na Woinde Shizza ,Arusha. 

Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kipindi cha kupiga kura ili kupata kiongozi bora ambaye anaweza kuiongoza serikali na kuiletea  nchi maendeleo kama vile Rais wa awamu ya tano John Magufuli alivyofanya.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa umoja wa jumuiya ya wazazi CCM, Edmund Mundolwa wakati akiongea na wananchi ,makadi wa Ccm wa halmashauri ya Meru alipofanya ziara ya kutembelea na kuona kuzindua rasmi mradi wa Nyuki uliopo katika Kijiji cha Sakila chini ,kata ya kikatiti pamoja na kutembea miradi mbalimbali ilotelekelezwa na serikali ya awamu ya Tano.
Alisema ni vyema wananchi wakajitokeza kwa wingi Siku ya kupiga kura ili kuweza kuchagua viongozi wao ambao wataweza kuwaongoza na kuwaletea maendeleo ,na sio kukaa nyumbani na kuacha kwenda kupiga kura ,kwani kupiga kura ni haki ya msingi ya kila mtanzania
Alisema kuwa katika uchaguzi ujao kwa upande wa Rais hawanashida kwani wananchi wenyewe wameshaona mambo mbalimbali aliyoyafanya katika kipindi chake cha uongozi kwani ameweza kufanya vitu Vingi ikiwepo kufufua shirika letu la ndege,kuturudishia reli ,kutengeneza barabara ,kuboresha huduma za Afya pamoja na kuboresha sekta ya Afya hivyo  kwa upande huo anawasiwasi.
Aidha alisema shughuli kubwa iliopo ni katika kuchagua wabunge na madiwani ambapo aliwataka wananchi kufanya maamuzi mazuri ya kuchagua mtu ambaye anaweza kufanya Kazi kuendana na kasi ya Rais ili aweze kuleta maendeleo yanayo onekana na sio kuwa mzigo kwa wananchi.
“Naweza sema Rais Magufuli  amekuja kwa wakati muhafaka katika nchi yetu ,kwani baada ya kupewa kiti tu amefanya mambo mengi ya maendeleo ,na ukiangalia alivyoingia  aliweza kuanza kufanya Kazi mambo mengi ambayo yalikuwa yanamkera na ndio maana alivyoanza Kazi tu alianza kurekebisha nchi yetu na alipoanza tu tumeona ata mapato ya nchi yameanza kuongezeka ata ukicheki kwenye magawio zamani tulikuwa kwenye milioni kadhaa sasa hivi tunapokea adi billioni” alibainisha 
Alisema ni kiongozi anaechukia ufisadi kiasi kwamba ameamua kuanzisha mahakama ya mafisadi ,nikiongozi ambaye ataki nchi iibiwe na ameweza kuthibiti mianya mingi ya wizi ,na anaamini watanzania hawakufanya kosa kumchagua kwani asingekuwa yeye ,ajui ata nchi yetu ingekuwa wapi kwa sasa .
Alibainisha kuwa alipoingia tu madarakani Magufuli alianza kwa kukamata makontena 3000 Bandari hivyo hiyo inaonyesha namna gani alikuwa anachikukia wizi ulikuwa unafanywa wakati akiwa waziri,hivyo kutokana na maendeleo ambayo ameleta kwa Taifa letu alimtaka kila mwananchi  kwa itikadi yake ya thehebu lake asiache kumuombea Rais wetu ili aendelee kuishi na kuongoza tena nchi yetu kwa miaka ijayo.
Akiongelea miradi hii ya Nyuki aliwataka viongozi wasimamie kwa uhakika kwani miradi hii italeta maendeleo kwa jumuiya ya wazazi na hata kwa nchi kwa ujumla ambapo aliwataka wenyekiti wote nchi Wa jumuiya za wazazi kupiga mfano Wa Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha Hezron Mbise ya kuongoza njia ya kuwaletea wananchi Wa wilaya zote za mkoa wa Arusha mizinga 100 kwa ajili ya mradi ya kutekeleza mradi huu.
Alimpongeza Mwenyekiti hiyo Wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha na kisema kuwa asiache tochi hii alianza izime bali aendelee kusaidia serikali  kuwaletea  wananchi maendeleo .
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa wazazi Herzon mbise alisema kuwa ameshatoa mizinga 700ya Nyuki ambapo kila wilaya ametoa mizinga 100 yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 20.