…………………………………………………………………………………
NJOMBE
Mamia ya watu wamejitokeza na kushiriki sara ya toba ambayo imeongozwa na viongozi wa madhehebu tofauti ya mkoa wa Njombe kwa lengo la kuombea tatizo la janga la ukimwi linaloutesa mkoa huo pamoja na maombi ya amani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Licha ya kushuka kwa kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 14.8 hadi 11.4 lakini mkoa wa Njombe umeendelea kuwa kinara kwa maambukizi kitaifa jambo ambalo linawasukuma viongozi wa dini kuwakumbusha wakazi wa njombe kurejea miguuni kwa muumba kutubu na kuombea amini idumu katika taifa hilo
Awali akifungua maombezi hayo mchungaji kiongozi wa kanisa la Fullgospel Nehemia Kabora na Mchungaji wa kanisa la Pentecoste Henrick Mwenda wanasema serikali imekuwa ikichukua jitihada lukuki kukabiliana na janga la ukimwi lakini akiri ya kibinadamu imeshindwa hivyo wakati umefika kukabidhi tatizo hilo kwa muumba asiyeshindwa na jambo .
Viongozi hao wanasema janga hilo limetokana na kukithiri kwa maovu ikiwemo mila potofu za kirithi wajane ,ulawiti na ubakaji jambo ambalo limemkasirisha mungu na kuamua kutoa adhabu kama ilivyokuwa SODOMA huku pia maombi mengine yakilenga kumuombea rais wa Tanzania na uchaguzi mkuu ujao.
Lillian Nyemele afisa tarafa Njombe mjini akitoa mwelekeo na mkakati wa serikali katika kukabiliana na janga la ukimwi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri anasema uamuzi wakuombea mkoa na taifa kuhusu janga la Ukimwi ni uamuzi mwema na kudai kwamba serikali itaendelea na mapambano ikiwemo kutoa elimu na matumizi ya kinga .
Baadhi ya wananchi na waumini wa madhehebu mbalimbali akiwemo Neema Chang’a wakizungumzia umuhimu wa misa hiyo ya toba wanasema itakuwa suruhisho la mikasa ya ajabu inayotokea Njombe kwani hata vitabu vya dini vinasema mungu humsamehe anaetubu.
Aidha Joshua Mbilinyi ambaye pia ni mchungaji anasema mungu hutoa adhabu kwa wanadamu pindi wanapozidisha uovu na wanapobaini makosa na kuamua kutubu pia husamee hivyo maombi hayo yatakuwa na matokeo chanya.
Mkoa wa Njombe umekuwa kinara wa Maambukiz ya ukimwi ,Udumavu huku mikasa mingine ya mauaji ikitokea mara kwa mara jambo ambalo limesukuma kufanyika ibada ya toba.