Home Mchanganyiko DC KILOLO ATOA TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA BARABARA KUU YA IRINGA NA...

DC KILOLO ATOA TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA BARABARA KUU YA IRINGA NA DAR

0

Tahadhari kwa watumiaji wa barabara kuu ya IRINGA-DAR kipande Cha Ruaha Mbuyuni zaidi eneo la darajani, inategemewa kuwepo na maji mengi kuanzia majira ya saa12 .

kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha ndani ya Wilaya na Maeneo mengineyo hivyo vyombo vya Usalama na Idara husika zitakuwepo eneo hilo la darajani muda wote mpaka maji yatakaporudi katika usawa wake wa kawaida .

Ili Kuepusha Madhara kwa watumiaji wa barabara hiyo. Kwa wakati huo Mabasi, Malori, Magari mdogo yataruhusiwa upande mmoja, watembea kwa miguu tunawaomba pia kuchukua tahadhari, Viongozi wa ngazi zote watapaswa kuhakikisha Watoto na wananchi kwa Ujumla wanakuwa mbali na eneo hilo.

Asia Juma Abdallah, DC-Kilolo, Mwenyekiti kamati ya Usalama Wilaya.