Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Mark Ocitti, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, Mashimba Ndaki (katikati) akiteta jambo na wanakamati wenzake muda mfupi baada ya kumaliza ziara yao ya kikazi katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Dar es Salaam jana
Meneja operesheni wa kampuni ya SICPA inayoendesha mfumo wa stempu za kielektroniki viwandani, Ibrahim Marwa (wa kwanza kushoto), akiwaelekeza jambo wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge waliotembelea kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Dar es Salaam jana.
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge wakiangalia namna uzalishaji bia unavyofanyika walipotembelea kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Dar es Salaam jana.
…………………………………………………………………………………………………….
Dar es Salaam
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge wamepongeza uwekezaji unaofanywa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) unaohusisha upanuzi wa kiwanda chake cha Dar es Salaam.
Kampuni ya SBL inafanya upanuzi wa kiwanda cha Dar es Salaam, moja kati ya viwanda vyake vitatu. Upanuzi huo unaogharimu Paundi za Uingereza milioni 10, utasaidia kuongeza uzalishaji wa bia ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya wateja wa kampuni hiyo.
Akiongea muda mfupi baada ya kutembelea kiwanda cha Dar es Salaam, mwenyekiti wa kamati hiyo Mahimba Ndaki alisema, uwekezaji huo utasaidia kutatengeneza ajira mpya kwa Watanzania na kuongeza mahitaji ya malighafi za kuzlisha bia kama shayiri, mahindi na mtama jambo ambalo litawaongezea wakulima kipato.
“Uwekezaji wenu endelevu unaenda sambamba na ajenga yetu ya Tanzania ya viwanda. Uwekezaji mkubwa kama huu unatia moyo na unaonyesha namna ambavyo mmejipanga vyema kutumia fursa zilizopo katika Tanzania ya Viwanda. Sisi tunawahakikishia ushirikiano wetu katika shughuli zenu za kila siku,” alisema Ndaki.
Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL John Wanyancha aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kwamba, upanuzi wa kiwanda hicho upo katika hatua za mwisho za kukamilika na kuongeza kuwa utasaidia kuongeza ajira pamoja na mapato kwa Serikali kupitia kodi.
Wanyancha aliongeza kuwa, kwa sasa SBL inanunua Shayiri, mahindi pamoja na mtama kutoka kwa wakulima wazawa kwa ajili ya uzalishaji wa bia zake na kwamba mwaka jana ilinunua tani za ujazo 17,000 sawa na asilimia 70 ya mahitaji yote ya malighafi ambayo SBL inatumia kwa mwaka
SBL imeajiri zaidi wa wafanyakazi 700 moja kwa moja na wengine maelfu kwa ajira zisizo za moja kwa moja kupitia mlolongo wa thamani ya biashara zake katika viwanda vyake vya Dar es Salaam, Moshi na Mwanza.