Mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dk. Agnes Kijazi akizungumza wakati akifungua semina ya waandishi wa habari leo katika makao mkuu ya taasisi hiyo kuhusu utabiri wa hali ya MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA KWA KIPINDI CHA MWEZI MACHI HADI MEI 2020 kushoto ni Dk. Hamza Kabelwa MKurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA.
Mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dk. Agnes Kijazi akifafanua jambo katika semina hiyo kushoto ni Dk Hamza Kabelwa MKurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA na kulia ni Willbeforce kikwasi Kaimu Meneja Ofisi Kuu ya Utabiri.
Mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dk. Agnes Kijazi akimsikiliza Dk Hamza Kabelwa MKurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA wakati akizungumza katika semina hiyo.
Mchambuzi wa hali ya hewa Abubakar Lungo akielezea jambo wakati akizungumzia rasimu ya utabiri wa MWELEKEO WA HALI YA HEWA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA KWA KIPINDI CHA MWEZI MACHI HADI MEI 2020.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dk. Agnes Kijaziakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina hiyo.
……………………………………………
Mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dk. Agnes Kijazi amefungua semina ya waandishi wa habari leo katika makao mkuu ya taasisi hiyo kuhusu utabiri wa hali ya MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA KWA KIPINDI CHA MWEZI MACHI HADI MEI 2020.
Akizungumza katika warsha hiyo Dk. Kijazi amesema huu ni muendelezo wa juhudi za mamlaka kuhakikisha taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa ikiwemo jamii kwa uhakika, usahihi na kwa wakati.
Amesema kwamba taarifa za hali ya hewa zikiifikia jamii kwa wakati, uhakika na usahihi itaisaidia jamii kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa pia itazisaidia mamlaka zinazohusika kupanga mipango endelevu ambayo haiwezi kuathiriwa na hali mbaya ya hewa.
Ameongeza kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ni ofisi pekee iliyopewa jukumu la kutoa huduma za hali ya hewa kwa jamii hapa nchini.
Mamlaka hii inahusika kutoa tahadhari za majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa yanayoathiri sana watu na mali zao. Majanga hayo huleta changamoto kubwa kwa wananchi hususan wakulima, wavuvi, wafugaji na wasafirishaji.
Ameongeza kuwa msimu unaokuja wa Machi hadi Mei 2020 ni msimu wa mvua katika baadhi ya maeneo hapa nchini hasa yale yanayopata misimu miwili ya mvua, vile vile ni msimu wa kilimo katika maeneo hayo; hivyo ni muhimu kwa wananchi na watumiaji wengine wa taarifa za hali ya hewa kupata taarifa sahihi na kwa wakati ili kuweza kujipanga na kujiandaa kabla ya msimu kuanza.
“Ili kufanikisha hilo, Mamlaka imekuwa ikihakikisha inakutana na wanahabari ambao ni daraja muhimu katika kuwafikia wananchi wote kwa ujumla ili kupata uelewa wa pamoja na namna bora ya kusambaza taarifa za hali ya hewa”. amesema Dk. Kijazi.
Kubwa la leo tumekutana kujadili MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA KWA KIPINDI CHA MWEZI MACHI HADI MEI 2020 na athari zinazoweza kujitokeza, hivyo wataalamu wameandaa rasimu ya mwelekeo huo na viashiria vilivyopelekea kupatikana kwa utabiri wa hali ya hewa kwa msimu wa mwezi Machi hadi Mei 2020.
Ni matumaini yangu kwamba majadiliano tutakayokuwa nayo hapa yatakuwa yenye tija katika sekta ya habari kwa maana ya uboreshaji wa njia za usambazaji wa taarifa za hali ya hewa.
Vile vile, kwa pamoja tutaangalia pia matokeo (performance) ya utabiri wa vuli jinsi ilivyotabiriwa na hali halisi ilivyojitokeza.
Dk. Kijazi amesema Mamlaka na Serikali kwa ujumla inatambua madhara yatokanayo na hali mbaya ya hewa nchini. Serikali imekuwa ikijitahidi kuijengea uwezo Mamlaka ya Hali ya Hewa kadri iwezekanavyo ili iweze kutekeleza vizuri majukumu yake na watumiaji wa taarifa za hali ya hewa wazipate mapema na kufanya maamuzi sahihi kwa wakati muafaka.
Amesema Mamlaka pia inatambua madhara yaliyotokana na hali mbaya ya hewa katika maeneo mbalimbali hapa nchini hivi karibuni. Madhara hayo ni kama vile mafuriko yaliyozikumba kaya mbali mbali katika mkoa wa Lindi na maeneo mengine nchini. Mamlaka inatoa pole kwa wote walioathirika na mafuriko hayo na kuwaomba watanzania wote wawe wanafuatilia taarifa za hali ya hewa pamoja na tahadhari zinazotolewa na TMA ili kupunguza athari zinazoweza kutokea.
Naendelea kusisitiza jamii kuwa bega kwa bega na TMA na kuepuka tabia ya kuwa na mazoea ya misimu ya hali ya hewa iliyozoeleka huko miaka ya nyuma, hasa ikizingatiwa kwamba mabadiliko ya tabia nchi yana athari katika mifumo ya hali ya hewa na hivyo kubadilika kwa misimu.