Mratibu wa mradi wa Instant Schools ulio chini ya Vodacom Tanzania Foundation, Christine Lucas akiongea na wana kamati na wazazi wa wanafunzi wa darasa la Tano wa Shule ya msingi Diamond jijini Dar es Salaam, kuhusiana na Program ya Soma Kidijitali ambapo mwanafunzi anapata masomo mbalimbali kupitia simu ya kiganjani, elimu hiyo ilitolewa kwa wazazi wakati wa kikao kilichofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki.