Mganga mfawidhi ya zahanati ya Kigoma Godlove Myinga akisoma taarifa ya maboresho yaliyofanywa na fedha za RBF kuanzia mwaka 2017 ikiwemo ujenzi wa wodi ya wazazi
Mganga mfawidhi wa zahanati ya Bangwe akimuelezea Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula jinsi walivyojipanga kutoa huduma endapo atatokea muhisiwa wa magonjwa ya mlipuko kwenye jengo maalum lililotengwa na manispaa ya kigoma
Dkt. Zainab Chaula akiangalia vifaa vilivyowekwa kwenye wodi hiyo maalum ya kuwahudumia wagonjwa wa milipuko endapo watatokea
Katibu Mkuu Dkt. Chaula akiongea na watumishi wa zahanati ya kigoma ambapo aliwasisitiza waongeza kasi ya kuwahudumia wananchi ambao wanafika.kupata huduma kwenye zahanati hiyo
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akiongea kwenye zahanati ya kigoma,amesema,kazi kubwa ya serikali ni kuwaendeleza watumishi wake hivyo alimuomba Mkurugenzi wa halmashauri ya kigoma Bw. Mwailwa Pangani kumuweka kwenye mpango wa kwenda kusoma mganga mfawidhi wa zahanati hiyo mwaka huu kutokana utendaji wake wa kazi
Mganga mfawidhi wa zahanati ya Bangwe, Praygod Willybad akimuelezea Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula jinsi walivyojipanga kutoa huduma endapo atatokea muhisiwa wa magonjwa ya mlipuko kwenye jengo maalum lililotengwa na manispaa ya kigoma
Jengo la wazazi ambalo limejengwa kutokana na fedha za malipo kwa ufanisi(RBF) ambapo imesaidia kuongezeka kwa akina mama kujifungulia kwenye zahanati kutoka akina wajawazito 10 kwa mwezi mwaka 2018 hadi akina wajawazito 30 kwa mwezi mwaka 2019
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kigoma Mwailwa Pangani akizungumza na watumishi wa zahanati ya kigoma (hawapo pichani)
Dkt. Chaula akikagua mazingira ya eneo lililotengwa kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko kwenye zahanati ya bangwe
Mratibu wa halmashauri ya wilaya ya kigoma wa uzazi wa mpango, baba, mama na mtoto Bi. Bernadetha Peter akitoa taarifa ya huduma ya mama na mtoto ya manispaa hiyo
………………………………………………
Na. Catherine Sungura-Kigoma
Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini
Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto-Idara kuu Aftlya Dkt. Zainab Chaula wakati akiongea na watumishi wa zahanati ya Kigoma jijini hapa.
“Tunaboresha huduma za afya kote nchini ili watu wasisafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya,zahanati ni ngazi ya awali ya afya ya msingi hivyo inasaidia wagonjwa wasio na shida kubwa kupata huduma karibu na maeneo yao”.Amesema Dkt. Chaula
Aidha, ameongeza kuwa kabla ya kuboresha huduma za afya nchini asilimia 80 ya akina mama walikuwa wakijifungulia majumbani,hivyo kwa hali.ya sasa akina mama wanafika vituoni kwa sababu ya kufuata huduma zilizoboreshwa.
Hali kadharika Dkt. Chaula aliupongeza Mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) kwa kuwajengea wodi ya wazazi kwenye zahanati na kuwapatia motisha watumishi
“Kigoma imeingia katika mpango huu mwaka 2017 na hivyo niwapongeze kwa kuweza kuboresha huduma pamoja na kufanya makubwa ,kwa maboresho haya lazima wananchi wapate huduma bila manyanyaso yeyote”.Alisisitiza
Naye Mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Godlove Myinga amesema kuwa kwa kipindi cha mwezi julai hadi septemba 2018 zahanati hiyo ilipokea kiasi cha shilingi milioni 7,924,214 ambazo asilimia 25 zitatumika kama motisha kwa watumishi na asilimia 75 itatumika kwa ajili ya ukarabati na vifaa tiba.
Kwa upande wa akina mama wanaojifungulia kwenye zahanati hiyo Mganga mfawidhi huyo amesema kumekuwa na ongezeko tangu wodi ya wazazi ilipozinduliwa mwaka 2018 kutoka akina mama 10 kwa mwezi hadi kufikia akina mama 30 mwaka 2019.
Mpango wa Malipo kwa Ufanisi (RBF) ni mfumo wa malipo ya fedha kwa vituo vya afya mara baada ya kufanyika uhakiki wa majukumu na viashiria vilivyowekwa na hivyo malipo hutokana na kiwango cha utendaji ,RBF ilianza kutekelezwa hapa nchini mwaka 2015 na kutarajia kuisha mwaka huu. Fedha za Mpango huu zimesaidia kuinua kiwango cha utoaji huduma katika vituo vya afya ambapo utumika katika kufanya ukarabati mdogomdogo wa vituo, ununuzi wa vifaa tiba, dawa na mahitaji mengine ya kituo.