Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akizungumza na viongozi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma kwenye kikao cha kufanya tathmini ya lishe mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2019/20 kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri ,Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri akizungumza kwenye kikao cha kufanya tathmini ya lishe mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2019/20 Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma
Afisa lishe kutoka Tamisemi Bw.Festo Filia,akitoa maoni kwenye kikao cha kufanya tathmini ya lishe mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2019/20 Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma
Sehemu ya washiriki wa kikao cha kufanya tathmini ya lishe mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2019/20 Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma
Ofisa lishe mkoa wa Dodoma, Heriet Carin,akitoa maada kwenye kikao cha kufanya tathmini ya lishe mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2019/20 Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma
Asifa utetezi na Mawasiliano Jukwaa la lishe nchini (PANITA),Faraja Kassima,akitoa elimu kwenye kikao cha kufanya tathmini ya lishe mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2019/20 Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma
Mganga mkuu wa mkoa Dk.Best Magoma,akijibu hoja mbalilmbai kwenye kikao cha kufanya tathmini ya lishe mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2019/20 Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akionyseha takwimu kuhusu lishe kwenye kikao cha kufanya tathmini ya lishe mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2019/20 ,Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akizindua kitabu cha makakti wa kukabiliana na utapiamlo na lishe kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano mara baada ya kufanyika kwa kwenye kikao cha kufanya tathmini ya lishe mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2019/20 kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Chemba, Simon Odunga ,Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
………………………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Halmashauri za mkoa wa Dodoma zimetakiwa kutenga fedha kwa ajili ya kukabiliana na utapiamlo na lishe kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,wakati akizungumza na viongozi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma kwenye kikao cha kufanya tathmini ya lishe mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2019/20
Dk.Mahenge amesema kuwa kila halmashauri imetenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kukabiliana na suala la lishe duni kwa akina mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka mitano lakini utekelezaji wake umekuwa ni mgumu.
“Kila Halmashauri inatakiwa kutenga sh 1,000 kwa ajili ya kukabiliana na utapiamlo kwa watoto walio chini ya miaka mitano lakini cha kusikitisha kuna baadhi ya Halimashauri hazitekelezi agizo hili hali inayoturudisha nyuma kwenye suala zima la mapambano dhidi ya utapiamlo,” amesema Dk.Mahenge
Aidha ametoa agizo kwa wale wote wanaohusika na utoaji wa mafungu ya fedha za kukabiliana na lishe kwa kila Halmashauri kufanya hivyo ili tukikutana tena mwezi wa sita mwaka huu tuwe tumefanya vizuri zaidi.
Awali Ofisa lishe mkoa wa Dodoma, Heriet Carin amesema kuwa jumla ya Sh 543.88 milion zilitengwa kwa ajili ya kukabiliana na utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano kwa mwaka 2019/20 lakini fedha zilizotolewa ni Sh 120.74 milioni ambazo ni sawa na asilimia 48 ya fedha yote iliyotengwa.
Bi.Carin amesema kuwa tathmini iliyofanywa na Mkoa ili kugundua watoto wenye utapiamlo mkali, udumavu na uzito mdogo uligundua kuwa kulikuwa na watoto 9,767 waliokuwa wanakabiliwa na suala la lishe duni mkoani hapa.
”Hivyo Halmashauri zote natazitaka zitoe kipaumbele katika masuala ya lishe kwenye bajeti zao ili kukomesha utapiamlo na kutengeneza kizazi chenye afya njema kwa maendeleo ya Taifa”amesema Bi.Carin
Kwa Upande wake Doris Munisi kutoka shirika lisilo la kiserikali la Delloite linaloendesha mradi wa lishe endelevu katika Wilaya sita za mkoa wa Dodoma aamesema kuwa wakiwa kama wadau muhimu wa afya watashirikiana na serikali ili kuhakikisha kuwa elimu dhidi ya lishe bora kwa ajili ya afya ya mama mjamzito na mtoto inatolewa ipasavyo.