***********************
NA EMMANUEL MBATILO
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni leo imewafikisha mahakamani watumishi watatu wa Manispaa hiyo kwa makosa tofauti kuomba na kupokea Rushwa kinyume cha sheria.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa takukuru mkoa wa kinondoni Bi. Theresia Mnjagira amesema mnano tarehe Januari 6 mwaka huu mtuhumiwa Elgibius Kamugisha ambaye ni karani wa ushuru wa soko la Kinondoni aliomba Rushwa ya sh. Laki tatu na kupokea sh. Laki mbili na elfu tano kutoka kwa mfanya biashara wa soko hilo ili amsaidie kutosumbuliwa na mpangaji wa awali wa eneo hilo la biashara.
Ameeleza Bi. Theresia katika tukio la pili mnamo tarehe 5 januari 2020 mtuhumiwa Judith Joseph afisa mtendaji wa mtaa wa maputo mbweni jijini hapa aliomba Rushwa ya kiasi cha sh. Laki tano na kupokea sh. Laki mbili na elfu themanini kutoka kwa mwananchi aliyehitaji kibali cha ujenzi.
Hata hivyo Bi. Theresia amesema katika tukio la tatu amesema mtuhumiwa Desdery Libury ambaye ni mhandisi wa manispaa ya Kinondoni aliomba rushwa ya sh. Milioni moja kutokabkwa mwananchi ili aweze kumpunguzia kulipa faini ya sh. Milioni 2 na elfu themanini na nane aliyotakiwa kulipa baada ya kujenga nyumba bila kibali cha ujenzi.
“Tunafanya kazi vizuri lakini wanaotoa taarifa wemekuwa wakitupatia ugumu wa kutokana na kutotoa ushirikiano mpaka mwisho”. Alisema Bi.Theresia.
Aidha, Bi. Theresia amewasihi wananchi kushiriki katika mapambanao ya Rushwa kwa kutoa taarifa za viashiria hivyo katika ofisi za TAKUKURU zilizopo karibu.