Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Uwezeshaji katika Kilimo (PASS Trust) imeendesha Kongamano maalumu la Wadau wa Sekta ya Kilimo cha Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyangakwa lengo la kuwapa elimu juu ya fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wakulima.
Kongamano hilo limefanyika leo Ijumaa Februari 7,2020 katika Ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga limewakutanisha wadau zaidi ya 400 wa sekta ya kilimo ikiwamo wakulima, vyama vya msingi vya wakulima (AMCOS), mashirika na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi kutoka mikoa hiyo.
Akifungua Kongamano hilo, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack ameipongeza CRDB kwa kuandaa kongamano hilo huku akiwataka wakulima kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na benki.
“Nimefurahishwa kusikia mwaka jana 2019 mmetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 650 kwenye sekta kilimo, hii inaonyesha ni jinsi gani mmedhamiria kushirikiana na Serikali kuleta mapinduzi kwenye sekta hii ambayo kimsingi ni sekta inayozalisha malighafi ya viwanda vyetu,” alisema Mhe. Telack.
Telack alisema Serikali kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, inaitambua sekta ya kilimo kama msingi imara katika kufikia uchumi wa kati wa viwanda.
Aliainisha baadhi ya maeneo ambayo Serikali imeyafanyia kazi ili kuboresha sekta ya kilimo ikiwamo uboreshwaji wa mfumo wa upatikanaji pembejeo za kilimo, uimarishwaji wa masoko ya mazao ya kilimo na uanzishwaji wa bima ya mazao.
“Nimefurahi kuona Benki ya CRDB kupitia huduma mnazotoa kwa wadau wa sekta ya kilimo kwa kiasi kikubwa huduma hizi zimegusia maeneo haya ambayo ndiyo msingi hasa wa kuboresha kilimo chetu,” aliongeza Mhe. Telack.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri aliwataka wakulima kufanya kilimo cha kisasa kwa kutumia zana na pembejeo za kisasa ili kupelekea kilimo chao kuwa na tija zaidi.
“Benki ya CRDB wametueleza hapa mikopo inayotolewa kumsaidia mkulima kuboresha kilimo chake, tumieni fursa hizi,” alisema Mwanri.
Naye Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Xavery Makwi alisema benki kupitia kauli mbiu yake ya ‘Tupo Tayari’ imejipanga vilivyo katika kuhakikisha inashirikiana na Serikali na wakulima kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini.
“Asilimia 40 ya mikopo yote ya kilimo nchini imetolewa na Benki ya CRDB, hii inaonyesha ni jinsi gani tumejikita katika kuwasidia wakulima lakini pia kuboresha uchumi kwani kilimo kinachangia zaidi ya asilimia 25 katika pato la taifa letu,” alisema Makwi.
Makwi alisema katika sekta ya kilimo Benki ya CRDB imekuwa ikitoa huduma za mikopo ya pembejeo, mikopo ya zana za kilimo, mikopo ya ujenzi wa maghala, uunganishwaji na masoko na uwekezaji kwenye viwanda.
“Mkulima anapofika tawini kwetu tunamfungulia akaunti ya FahariKilimo, hii ni akaunti maalum kwa ajili ya wakulima, haina makato ya aina yoyote na hufunguliwa bure,” aliongeza Makwi.
Makwi alisema kuwa tayari wakulima zaidi ya 30,000 nchi nzima wameshajiunga na akaunti ya FahariKilimo, na kuunganishwa na huduma za uwezeshaji kupitia mikopo inayotolewa na Benki ya CRDB.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi,Saidi Pamui aliwashauri wakulima wa pamba kufungua akaunti benki ya CRDB ili waweze kulipwa pesa zao kupitia benki.
“Lengo la CRDB ni kufanya biashara moja kwa moja na AMCOS ili tuweze kuwakopesha kwa urahisi wakulima wa pamba. Ili kufikia lengo hili tutaenda kufungua akaunti kwa wakulima bure,tutampa kadi mkulima bure, tutamfungulia sim banking burena wakati wa malipo kama mawakala wetu watakuwa hawatoshi tupo tayari kuleta wafanyakazi wetu ili wafanye malipo haraka”,alisema Pamui.
Meneja wa PASS Trust Kanda ya Ziwa, Langelika Kalebi aliwataka wakulima kuitumia vizuri taasisi hiyo hususani katika kuandaa mpango wa kilimo na uongezaji wa thamani wa dhamana ikiwa ni vitu muhimu vinavyohitajika wakati wa uombaji wa mikopo katika taasisi za fedha.
Wadau wa kilimo waliohudhuria kongamano hilo wameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuboresha upatinikanaji wa huduma zake hasa vijijini, kupitia CRDB Wakala zaidi ya 14,000 nchi nzima ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kufikisha huduma za Benki karibu zaidi na wateja.
“Sisi wakulima tunapatikana mashambani, hivyo uwepo wa CRDB Wakala umesaidia sana kutuwezesha kutumia akaunti zetu za FahariKilimo kwani sasa hivi hatuhitaji kutembea umbali mrefu,” alisema mmoja wa wakulima waliohudhuria kongamano hilo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akifungua Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust leo Ijumaa Februari 7,2020 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri.Wa Kwanza kulia ni Meneja wa PASS Trust Kanda ya Ziwa, Bi. Langelika Kalebi akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi,Bw. Saidi Pamui. Picha zote na Kadama Malunde
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akifungua Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Wadau wa kilimo cha pamba wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack. Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akizungumza wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akiishukuru Benki ya CRDB kwa kukutanisha pamoja wadau wa pamba.
Wadau wa kilimo cha pamba wakiwa ukumbini.Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Xavery Makwi akizungumza wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Xavery Makwi akizungumza wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi,Saidi Pamui akizungumza wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Meneja wa PASS Trust Kanda ya Ziwa, Langelika Kalebi akizungumza wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Xavery Makwi na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi,Saidi Pamui (kulia).
Kongamano linaendelea.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Meneja Mahusiano benki ya CRDB,Kilo Mgaya akizungumza wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri baada ya kufungua Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust. Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU),Emmanuel Charahani akizungumza wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Mnunuzi wa Pamba ,Bryson Edward kutoka Kahama Oil Mill (KOM) akizungumza wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyang’hwale,Mhe,. Mariam Chaurembo akizungumza wakati wa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Meneja Mwandamizi Ukusanyaji Amana Binafsi benki ya CRDB, Abel Lasway akitoa mada kwenye Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba na kuwaeleza fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB.
Afisa wa Benki ya CRDB Japhar Othman kutoka kitengo cha Mawakala akielezea fursa zinazotolewa na benki ya CRDB.
Meneja Mwandamizi Uwezeshaji Benki ya CRDB,Malegesi Shaban akiwasisitiza wakulima kufungua akaunti benki ya CRDB.Mdau wa pamba kutoka Kakonko mkoani Kigoma,Sabas Silvanus akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Mdau wa pamba kutoka Igunga Tabora,Adelina Blazi akichangia hoja wakati wa kongamano hilo.
Kongamano linaendelea. Kongamano linaendelea.
Kongamano linaendelea.
Kongamano linaendelea.
Kongamano linaendelea.
Kongamano linaendelea.
Wadau wa pamba wakiwa ukumbini.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi,Saidi Pamui akizungumza wakati wa kufunga Kongamano la Wadau wa Sekta ya Pamba kutoka Mikoa ya Geita,Kigoma,Tabora na Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na PASS Trust.
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri, wafanyakazi wa benki ya CRDB,Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha,Meneja wa PASS Trust Kanda ya Ziwa, Langelika Kalebi na wafanyakazi wa serikali
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri, wafanyakazi wa benki ya CRDB,Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha,Meneja wa PASS Trust Kanda ya Ziwa, Langelika Kalebi na viongozi wa vyama vya ushirika.
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri, ,Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha,Meneja wa PASS Trust Kanda ya Ziwa, Langelika Kalebi na wafanyakazi wa benki ya CRDB.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog