***************************
NA EMMANUEL MBATILO
JKT TANZANIA yafanikiwa kuibamiza klabu ya Simba bao 1:0 katika dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la ushindi limefungwa na Adam Adam dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza ambalo limedumu mpaka mwisho wa kipindi.
Nyota wapya wa Simba, Luis na Shiza Kichuya wameanza leo kwa mara ya kwanza.
Mchezo wa kwanza walipokutana Simba ilishinda mabao 3-1 na leo kisasi kimelipwa kwa JKT kushinda bao 1-0.