……………………………………………………………………………………………………..
Na Silvia Mchuruza,Missenyi,Kagera
Takribani wananchi elfu 54 na 554 wilayani missenyi mkoani kagera wameshindwa kusajili laini zao kwa alama za vidole kutokana na kushindwa kupata namba zao za kitambulisho cha taifa zinazotolewa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa baada ya taarifa zao kuwa na utata.
Katika taarifa iliyotolewa na katibu tawala wilayani humo kwa niaba ya ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo na kusomwa na afisa mipango wilayani humo ALBERT MSEMO mbele hya baraza la madiwani,ilieleza kuwa mpaka sasa wananchi waliopata namba za kitambulisho cha taifa ni elfu 18 na 388.
Ameongeza kuwa makadirio yalikuwa kuandikisha watu elfu 88 na 889 katika kata 20 za wilaya hiyo ambapo mpaka sasa wameandikishwa jumla ya watu elfu 79 na 109 huku waliobaki wakiwa elfu 12 na 60.
Aidha baadhi ya madiwani akiwemo AMUD MIGEYO na IBRAHIM KAISLANGA wameiomba serikali kuitaka mamlaka ya mawasliano Tanzania TCRA kusitisha zoezi la kuzima laini za simu za watu ambao hawajakamilisha usajili kwani wamekuwa wakishinda kwenye ofisi za NIDA kufuatilia taarifa zao bila mafanikio.