Baadhi ya vitu vya asili kutoka Makunduchi,ukiwemo Msikiti Kichaka, vyakula na kupigana magomba, vilifanywa katika Tamasha la Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud wa kwanza (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa mwakakogwa Mzee Mwita wakati wakiwa katika ziara ya Tamasha la Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja.
Mmoja wa Washiriki wa Tamasha la Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja Kudrat Mussa kutoka Tanzania Bara akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha hilo na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Kiboje Wilaya ya kati.
Fundi Mkuu wa Baskeli katika msafara wa Tamasha la Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja Juma Lukodwa akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha hilo na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Kiboje Wilaya ya kati.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akimkabidhi Cheti cha ushiriki wa Tamasha la Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli Vuai Ali Maneno kutoka Vilabu vya Baskeli Zanzibar hafla iliyofanyika Kiboje Mkoa wa Kusini Unguja
Sheha wa Shehia ya Cheju Bitatu akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha la Utalii wa Baskeli na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud katika Ufungaji wa Tamasha hilo huko Kiboje Wilaya ya Kati.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi Baraza la Vijana la Wilaya ya kati Baskeli na Vifaa vya kazi huko Kiboje Wilaya ya kati katika Ufungaji wa Tamasha la Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja.
Baraza la Vijana kutoka Wilaya ya Kusini Unguja wakikabidhiwa Baskeli na Vifaa vya kazi na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud hafla iliyofanyika Kiboje Wilaya ya kati.
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………………………….
Na Mwashungi Tahir Maelezo
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud ameitaka jamii kutembelea vivutio vya utalii ili kuelewa vivutio vya kitalii viliopo Zanzibar na kuachana na dhana ya utalii kwa wageni .
Akizungumza hayo na Washiriki wa Tamasha la Utalii wa Baiskeli huko Shehia ya Kiboje Mkoa wa Kusini Unguja wakati alipokuwa akifunga tamasha hilo na kuitaka jamii , vijana kutembelea sehemu zenye mambo mbalimbali katika Mkoa huo.
Amesema Wazanzibar wengi wanahisi utalii uko sehemu ya Forodhani , na kuwataka waachana na dhana hiyo, kwa kufahamu kwamba utalii uko Zanzibar nzima na una sehemu nyingi za vivutio takribani vingi sana ikiwemo Mkoa wa Kusini Unguja.
“Watalii wengi wanaona utalii upo Forodhani tu, hapana, utalii uko Zanzibar Nzima na kuna vivutio vingi katika sehemu mbali mbali za Zanzibar”, Alisema Mkuu wa Mkoa huyo.
Hata hivyo amesema wazaliwa wa Nchi hii wawe wa mwanzo katika kukuza utalii wa ndani na kuutangaza Utalii kwa wote na ili uwe endelevu kwa lengo la kuuimarisha.
Aidha aliwataka Wazanzibar kuweka mashirikiano na umoja kwa lengo la kuuweka utalii wa ndani na utalii kwa wote katika Mkoa huo.
Pia alisema katika Mkoa wa Kusini Unguja tushatekeleza kwa vitendo dhana hiyo ya Utalii kwa kufanya matembezi katika maeneo mbali mbali ya kitalii yenye vivutio vyote vya Kitalii na kuwapatia fursa vijana kuweza kujua mambo yaliyomo .
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana Mustafa amesema rasilimali zilizopo ndani ya Mkoa huo zitawafanya vijana kuzitumia kwa kupitia ujasiriamali na mambo mengine ya kujiendeleza kwa kupitia vivutio hivyo vya utalii.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kati Hamida Mussa Khamis amesema lengo kuu la Tamasha hilo ni kuunga mkono Jitihada za Serikali ya Mapinduzi katika Sekta ya Utalii wa ndani na Utalii kwa wote kwa kufanya kwa vitendo.
Pia amesema ndani ya tamasha hilo vijana wameweza kujifunza na kuelimika kwa mambo mengi ambayo walikuwa hawayajui.
Nao washiriki wamevutika sana kwa matembezi hayo na kuahidi mwakani watajitokeza zaidi.
Zaidi ya vivutio vya utalii wa ndani na Utalii kwa wote 13 vimeweza kutembelewa na washiriki kukabidhiwa vyeti na Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tena ifikapo Ijumaa ya mwisho January 2021 ndani ya Mkoa huo