Home Mchanganyiko RC TABORA APOKEA VIFAA TIBA NA UJENZI VYENYE THAMANI YA MILIONI 19.8...

RC TABORA APOKEA VIFAA TIBA NA UJENZI VYENYE THAMANI YA MILIONI 19.8 KUTOKA ALLIANCE ONE

0

IMG_0120.JPG

IMG_0136.JPG

vlcsnap-2020-02-02-14h33m14s52.png

vlcsnap-2020-02-02-14h33m24s211.png

vlcsnap-2020-02-02-14h34m02s2.png

vlcsnap-2020-02-02-14h34m28s114.png
Mkuu wa Mkao wa Tabora aggrey Mswanri(kushoto) akipokea jana vifaa tiba kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kampuni ya Alliance One Tanzania Limited  David Mayunga (kulia) 

……………………………………………………………………………………………………………

NA, TIGANYA VINCENT, TABORA.

KAMPUNI ya Tumbaku ya Alliance One Tanzania (AOTTL)  imeukabidhi uongozi wa Mkoa wa Tabora vifaa mbalimbali vikiwemo vifaa tibaa na ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 19.8.

Msaada huo umekabidhiwa leo na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kampuni hiyo David Mayunga kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri katika halfa iliyofanyika Ofisini kwake.

Mayunga alivitaja vifaa vilivyotolewa ni Bati 200, Saruji mifuko 250, magodoro 30, shuka za wagonjwa 110, vitanda vya wagonjwa 3 na kitanda maalumu kwa ajili ya mama kujifungulia kimoja.

Alisema msaada huo utapelekwa katika Kituo cha Afya cha Mazinge na Kituo cha Afya cha Mwamayunga vilivyopo wilayani sikonge na Zahanati ya Igagala wilayani Kaliua.

Mayunga alisema Kampuni hiyo imeamua kutoa msaada huo kupitia mpango wa ujerejeshaji wa huduma kwa ili kuunga mkoano juhudi za Serikali za kuboresha huduma za afya na kuwapunguzia adha wananchi wa kwenda kupata huduma hizo mbali.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri aliitaka Idara ya Afya ya Mkoa huo kuhakikisha vifaa hivyo vinatunzwa na kutumika kwa malengo ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Alionya kuwa hatasitakuchua hatua kwa watendaji wote waliopewa dhamana ya kutunza vifaa kuhakikisha haviibiwi na kupelekwa kwenye majumba ya watu au kwa watoa huduma ya afya ambao sio walengwa.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama aliishukuru Kampuni ya Alliance One kwa msaada ya vitanda walivyotoa kwa ajili ya kuongezea nguvu Zahanati ya Igagala.

Alisema hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na msongamano wa kupata vifaa vya kulaza wagonjwa katika Zahanati hiyo.

Busalama alisema kutokana na Zahanati hiyo kupata wagonjwa wengi kutoka sehemu mbalimbali wanao mpango wa kujenga Kituo cha afya katika eneo hilo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua , nguvu za wananchi na kuomba wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo.