Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila wakati akifungua semina ya watendaji wa mamlaka husika kuhusu uendelezaji,uchimbaji wa madini ya urani na usalama wake iliyofanyika kwenye jengo la TACAIDS jijini Dar es salaam leo.
Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila wakati akifungua semina ya watendaji wa mamlaka husika kuhusu uendelezaji,uchimbaji wa madini ya urani na usalama wake iliyofanyika kwenye jengo la TACAIDS jijini Dar es salaam leo kulia ni Mkurugenzi Prof. Lazaro Busagala Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)
Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila wakati akifungua semina ya watendaji wa mamlaka husika kuhusu uendelezaji,uchimbaji wa madini ya urani na usalama wake iliyofanyika kwenye jengo la TACAIDS jijini Dar es salaam leo kulia ni Mkurugenzi Prof. Lazaro Busagala Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ,Danny Nyambo
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya watoa mada kutoka jumuiya ya Ulaya wakiwa tayari kwa kutoa mada katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo kutoka wizara na taasisi mbalimbali walioshiriki katika semina hiyo.
Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo baada ya kuifungua rasmi leo.
…………………………………………………
Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila amesema mpaka sasa , wizara ya madini imetoa leseni moja tu kwa kampuni ya Mantra ili kuchimba madini lakini hata hivyo uchimbaji wake haujaanza kutokana na kutokamilisha vigezo na masharti ya sheria.
Prof Simon Msanjila ameyasema hayo wakati akitoa msimamo wa Serikali kuhusu uchimbaji wa madini ya Urani kwa ajili ya nishati mbadala wakati akifungua semina ya watendaji wa mamlaka husika kuhusu uendelezaji,uchimbaji wa madini ya urani na usalama wake,
Amesema madini hayo yataanza kuchimbwa baada ya kampuni ya Mantra iliiliyopewa leseni kukamilisha sheria na taratibu walizotakiwa kuzitekeleza na serikali.
Amesema itafika wakati kampuni hiyo itakidhi vigezo na wataanza kuchimba na kuendeleza madini hayo yaliyogundulika kwa wingi katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma hivyo lazima nchi kuanza kujiandaa na kuandaa wananchi kwa kuwapa uelewa kuhusu madini hayo.
“Tunajua madini haya yanaweza kutumika kwa nia nzuri kama kuzalisha nishati na nia nyingine ikiwemo kutengeneza silaha na mabomu lakini kama nchi bado msimamo wetu wa kuzalisha nishati kwa njia mbadala hivyo uchimbaji wa madini ya urani utafuata sheria inayosimamia madini mengine”alisema Profesa Msanjila
Katibu Mkuu amesisitiza kuwa ufahamu kwa watanzania kuhusu mazingira na usalama unaoendana na uchimbaji na matumizi ya urani utasaidia kuwa waelewa na ikifika wakati yakianza kuchimbwa wawe wameishajua yanavyochimbwa na usalama wao.
“Kuna umuhimu wa kuhakikisha elimu kwa wananchi inafanikiwa kwani madini hayo uchimbaji wake unatakiwa kufanyika kwa uangalizi wa pamoja huku raia wanatakiwa kuelewa faida na madhara ya madini kama yasipochimbwa kwa umakini kwa kufuata taratibu za usalama”amesema
Alisema utakapofika wakati wa uchimbaji wa madini hayo na kubainika kuna uhitaji wa kutungia sheria nyingine zitatungwa kwa wakati huo kuangalia manufaa ya nchi na watanzania.
Naye Mkurugenzi Mwezeshaji wa Kampuni ya Mantra Tanzania iliyopewa leseni ya kuchimba madini hayo, Frederick Kibodya alisema licha ya kukamilika kwa baadhi ya taratibu uchimbaji wa madini hayo utafanyika baada ya bei katika soko la dunia kufikia kiwango cha kulipa gharama za uendeshaji kwani kwa sasa bei iko chini ziko chini ambapo wanatarajia bei kuongezeka baada ya miaka mitatu hadi minne.
Alisema kwa makadirio inaonekana bei katika soko la dunia itafikia kiwango stahiki baada ya miaka mitatu hadi minne na kuanza uzalishaji katika eneo hilo la Namtumbo mkoani Ruvuma.
Alisema baada ya utafiti wa kina kuhusu mradi huo kwa sasa wanachofanya ni kuuendelezwa kwa ajili ya uzalishaji na maandalizi ya msingi tayari yamekamilika ikiwemo kupata vibali ambavyo ni kibali kutoka wizara ya Madini,Kibali cha mazingira kutoka Baraza la taifa la Hifadhi ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) .
“Bado kibali cha mazingira kutoka wizara ya maliasili na utalii kutokana na kuwa baadhi ya sehemu yalipogundulika madini hayo yapo katika hifadhi ya taifa ya selous iliyopitishwa hivi karibuni “Alibainisha