Home Michezo SPIKA NDUGAI KUZINDUA TAWI LA WABUNGE MASHABIKI WA SIMBA

SPIKA NDUGAI KUZINDUA TAWI LA WABUNGE MASHABIKI WA SIMBA

0

Mwenyekiti wa Mashabiki wa Simba wabunge Mhe.Rashid Shangazi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu uzinduzi wa Tawi Jipya la WEKUNDU wa MJENGONI pamoja na Uzinduzi wa Kadi za Mashabiki zoezi hilo litafanyika kesho  jijini Dodoma.

Mhamasishaji wa mashabiki wa Simba ambao ni wabunge Mhe.William Ngeleja  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya  uzinduzi wa Tawi Jipya la WEKUNDU wa MJENGONI litakalozinduliwa kesho kwenye viwanja vya bungeni.

Mashabiki wa Simba Mhe.Salome Makamba (kulia),akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwahamasisha Mashabiki wote waliopo Dodoma na nje ya Dodoma kujitokeza kwa wingi katika  uzinduzi wa Tawi Jipya la WEKUNDU wa MJENGONI pamoja na Uzinduzi wa Kadi za Mashabiki zoezi hilo litafanyika kesho  jijini Dodoma.

Wabunge Mashabiki wa Simba wakiwa karika picha ya pamoja mara baada ya kutoa taarifa kuhusu uzinduzi wa tawi pamoja na ugawaji wa kadi kwa mashabiki.

PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG

…………………………………………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Spika wa bunge Mhe.Job Ndugai anatarajia kuzindua tawi la wabunge mashabiki wa Simba liitwalo WEKUNDU WA MJENGONI  ambapo mwenyekiti wa tawi hilo Mhe.Rashid Shangazi amewaita mashabiki wa klabu hiyo kuchukua kadi za Uanachama.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mwenyekiti wa timu hiyo Mhe.Rashid Shangazi amesema kuwa uzinduzi huo utaambatana na uzinduzi wa kadi za mashabiki, wapenzi pamoja na wanachama maeneo ya  Equity Bank tawi la Dodoma lililopo Uhindini.

Aidha Mhe.Shangazi amesema kuwa katika tukio kubwa na la kihistoria kwa wabunge kuwa na Tawi amewaomba watani zao Yanga kujumuika nao ili nao waweze kujifunza hata kuiga mambo yaliyo mazuri.

”Tumewaalika mashabiki wote wa Yanga akiwemo Waziri Mhe.George Mkuchika ambaye ni Mdhamini wa Yanga,Mbunge wa Dodoma Mhe.Anthony Mavunde,Freeman Mbowe pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Muroto”amesema Shangazi.

Naye Mhamasishaji wa klabu hiyo Mbunge wa Sengerema Mhe.William Ngeleja,amewaomba mashabiki na wapenzi pamoja na wanachama wote kanda ya Dodona kujitokeza kwa wingi kwenye tukio hili muhimu kwa faida ya timu.

”Dunia kitu kinachopendwa zaidi na mpira wa mguu na sisi kama mashabiki wa Simba tumekuwa wabunge wa kwanza nchini pamoja na Duniani kuwa na Tawi jipya na la Kisasa”

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe.Salome Makamba,amesema kuwa Simba ni klabu kubwa na yenye mafanikio hapa nchini hivyo wameamua kuiunga mkono katika uzinduzi huu wa tawi pamoja na ugawaji wa Kadi kwa Mashabiki.

Kwa upande wa klabu ya Simba wataongozwa na Mtendaji Mkuu Senzo Mbatha pamoja na Msemaji wa klabu hiyo kipenzi cha wanasimba Haji Manara atakuwepo kwa ajili ya kuhamasisha zoezi hilo la kihistoria