Home Mchanganyiko DAR ES SALAAM KUADHIMISHA WIKI YA MAHAKAMA KWA KUTOA MSAADA WA KISHERIA...

DAR ES SALAAM KUADHIMISHA WIKI YA MAHAKAMA KWA KUTOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI BURE.

0

*********************************

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda anawaalika wananchi wote wa Mkoa huo wenye Kero za kisheria kujitokeza kwa Wingi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Mahakama yanayotaraji kuanza February 01 hadi 05 kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja.

RC Makonda kwa kushirikiana na Mahakama kuu ya Kanda ya Dar es salaam wameandaa wataalamu wakiwemo Mawakili, Wanasheria, Jeshi la polisi Dawati la Jinsia, Jeshi la Magereza, Chama cha Wanasheria Tanganyika pamoja na wadau wa kisheria wa kutosha kuhakikisha kila mwananchi anaefika kwenye viwanja hivyo anapata huduma stahiki ya kisheria pasipo usumbufu wowote.

Maadhimisho ya Wiki ya Mahakama yatatanguliwa na Maandamano yatakayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kuanzia Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam hadi viwanja vya Mmoja mapema Asubuhi.

Walengwa wa Zoezi hilo ni Wananchi wenye kero za migogoro iliyopo Mahakamani, Mienendo ya kesi, Wale ambao hukumu zao zimetoka na wanataka kukata rufaa lakini hawapewi nakala za hukumu kwa maandishi, Wananchi wasiojua wapeleke wapi kesi zao, Malalamiko ya maabusu, Polisi pamoja na kesi za ukatili wa kijinsia.