Home Mchanganyiko FAMILIA YA MWANAIDI KAMBI YATANGAZA KUPOTEA KWA NDUGU YAO AKIM SALEHE MSAKATILE 

FAMILIA YA MWANAIDI KAMBI YATANGAZA KUPOTEA KWA NDUGU YAO AKIM SALEHE MSAKATILE 

0

********************************

FAMILIA  ya Mwanaidi Kambi wa mtaa wa Somali wa Kipande, Gerezani jijini Dar es Salaam imesema inasikitika kutangaza kupotea kwa ndugu yao mwana Gerezani Akim Salehe Msakatile(50), ambaye alitoweka nyumbani kwake Magomeni Mapipa mtaa wa Dosi siku ya Jumatatu ya Januari  13 mwaka 2020.

Kwa mujibu wa familia hiyo ndugu yao alipotea saa mbili  usiku ambapo alitoweka na gari aina ya Ractis.Hata hivyo gari lilipatikana siku iliyofuatia ya Jumanne likiwa limetelekezwa maeneo ya Jangwani karibu na kituo cha mwendokasi. 

Imesema kuwa mara ya mwisho alikuwa amevaa kaptula (double pocket) na shati jeupe lenye maua madogo na kwamba mpaka inapotoka taarifa hii leo Januari 27 bado ndugu tajwa hajapatikana.

“Hivyo familia tunaomba kwa yoyote atakae kuwa na taarifa zake atoe taarifa kituo chochote cha polisi au awasiliane kwa namba 0655716767 au 0655338333 ama 0716565412,”imesema taarifa ya familia hiyo.