Mkurugenzi wa Kinga na Daktari bingwa magonjwa ya saratani wa Taasisi ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ,Dkt. Crispin Kahesa akifungua semina ya wahariri wa vyombo vya habari kuhusu magonjwa ya Saratani iliyofanyika kwenye taasisi ya Saratani ya Ocean Road leo jijini Dar es salaam katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi hiyo,Dkt.Mark Mseti na kushoto ni Dkt. Maguha Stephano Meneja wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani (OCRI)
Mmoja wa watu waliowahi kuugua Saratani na kutibiwa Mama Kuzilwa akitoa ushuhuda wake ambapo amewataka wananchi wanaougua au kuona dalili za Saratani waende hospitali mapema ili kupata tiba.
Dkt. Maguha Stephano Meneja wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani (OCRI) akifafanua jambo katika semina hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi hiyo,Dkt.Mark Msetiakitoa mada kuhusu magonjw aya Saratani wakati wa semina hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Kinga na Daktari bingwa magonjwa ya saratani wa Taasisi ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ,Dkt. Crispin Kahesa na kushoto ni Dkt. Maguha Stephano Meneja wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani (OCRI).
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo.
……………………………………………..
WITO umetolewa kwa watanzania kuondokana na imani potofu pindi wanapoumwa magonjwa ya Saratani na kuacha kwenda kwa waganga wa kienyeji bali kukimbilia hospitali kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Kinga na Daktari bingwa magonjwa ya saratani wa Taasisi ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ,Dkt. Crispin Kahesa alisema asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo wanakuwa tayari wamefika katika hatua za mwishoni.
Amesema wagonjwa wamekuwa wakidanganywa juu ya dawa za saratani hivyo wengine kuacha kuja hospitali na kwenda kwa waganga wa kienyeji hadi wanapofika hatua za mwisho.
Pia Dk.Kahesa amesema kwa sasa hali ya magonjwa ya saratani yamekuwa yanaongezeka na kubadilika kutoka katika virusi na kuwa saratani inayotokana na mfumo wa ulaji chakula .
Dk.Kahesa amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika hospitali yao kfanya uchunguzi wa saratani bila malipo yeyote.
Alisema katika maadhimisho hayo ambayo kilele chake kinatarajiwa kuwa Februari 4 mwaka huu,hospitali hiyo imeanza kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti,Saratani ya shingo ya kizazi,Tezi Dume na Uchunguzi wa Homa ya ini kuelekea katika siku ya kilele ya maadhimisho hayo.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi hiyo,Dkt.Mark Mseti alisema saratani ni kundi la magonjwa yasioambukiza .
Amesema saratani zinazoongoza katika taasisi hiyo ni pamoja na saratani ya Shingo ya Kizazi,Matiti,Ngozi ya Kapoji Sarcoma,Koo la Chakula na Saratani ya kichwa na Shingo.
Amesema kuwa tiba ya mionzi kwa sasa inatolewa katika hospitali zote za Kanda zikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Benjamin Mkapa ya Dodoma, Bugando Mwanza, KCMC Kilimanjaro na Ocean Road Yenyewe ambayo inatoa tiba ya miozni na matibabu mengine ya kibingwa kwa magonjwa ya Saratani.