Daraja la Koga likiwa likiwa limefunikwa na maji ya mvua
Stendi kuu ya Mizengo Pinda iliyoko katika Manispaa ya Mpanda
************************
Na Mwandishi wetu, Katavi
Kufungwa kwa kwa barabara ya Mpanda-Tabora; abiria wapungua
Stendi kuu ya Mizengo Pinda iliyopo katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imepata changamoto ya kudorora kwa biashara na kupungua kwa abiria wanaotumia stendi hiyo kuelekea mikoa mingine
Abiria wanaotoka Mpanda kuelekea mikoa ya Mwanza, Tabora, Geita, Shinyanga na Arusha wamepungua kutokana na kufungwa kwa barabara kuu ya Mpanda Tabora baada ya daraja Koga kujaa maji kiasi cha kushindwa kuonekana hali iliyolazimu uongozi wa mkoa wa katavi kufunga barabara hiyo
Wakizungumzia hali hiyo baadhi ya abiria waliokutwa katika stendi hiyo walisema nauli zimeongezeka kutokana na kupita njia ya mzunguko ambayo ni Uvinza mkoani Kigoma ili kufika Tabora
“Nilikuja hapa na 35,000/= ambayo ni nauli ya Mpanda hadi Mwanza sasa nimelipa 45,000/=” alisema mmoja wa abiria hao
Aidha baadhi ya mawakala wa makampuni ya mabasi walisema kutokana na abiria kupungua mabasi maengine yamesitisha safari zake mpaka barabara itakapofunguliwa
“Huku uvinza tunaongeza kilometa 155 kutoka 370 mpaka kufika Tabora, gharama inaongezeka abiria wenyewe wachache imebidi matajiri kushindwa!” alisema Athanas Julius ambaye Mwenyekiti wa Wasafirishaji mkoa wa Katavi
Mwishoni mwa wiki iliyopita Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga aliifunga barabara ili kuepuka madhara ambayo yangeweza kutokea
Pia aliwataka watumiaji wa barabara hiyo kupitia Uvinza ama kutumia njia nyingine za usafiri kama reli na ndege