Kamanda wa Polisi Dodoma  Girres Muroto,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo ofisini kwake wakati akitoa taarifa za matukio kwenye mkoa wake.

Kamanda wa Polisi Dodoma  Girres Muroto,akionyesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa katika matukio ya wizi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo ofisini kwake wakati akitoa taarifa za matukio kwenye mkoa wake.

…………………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma
Jeshi la Polisi Mkoa wa  Dodoma limemkamata  Boniface  Mushi  ambaye
ni mlinzi  wa Ofisi za TANESCO  baaada  ya kuvunja ofisi za hizo
eneo la area D jijini Dodoma   na kuiba kompyuta mpakato[Laptop].

Akizungumza na waandishi wa habari leo  jijini
Dodoma,Kamanda wa Polisi mkoani hapa Girres Muroto   amesema msako
mkubwa  ulifanyika katika eneo hilo  ambapo mlinzi wa kampuni binafsi
ya ulinzi  QSS   Deus Mushi  alikamatwa katika eneo la wilaya ya
Kwimba Mkoani Mwanza  baada ya kuiba laptop hiyo kutoka Dodoma  katika
ofisi za TANESCO,  za mradi wa miundombinu  ya umeme  shirikishi ya
nchi tatu  ambazo ni Tanzania ,Kenya na Zambia.

Katika tukio jingine kamanda Muroto amesema  katika Mtaa wa Kizota
jijini Dodoma  alikamatwa Joshua Elisha [38] mlinzi wa Kampuni ya
ulinzi ya KK Security  mkazi wa     Kizota Mbuyuni  akiwa na
Copresssor ya  friji kubwa ambayo ni mali ya wizi  aliyoiba baada ya
kuvunja  store ya lindo .

Aidha,Kamanda Muroto amesema  jeshi hilo limeokota Jumla ya pikipiki
nne katika maeneo tofauti   zikiwa zimetelekezwa na wahalifu wakati wa
doria  ambapo wenye pikipiki walikimbia baada ya kukurupushwa  wakiwa
kwenye harakati za kufanya uhalifu na pikipiki hizo ni MC.813 CDH
Fekon nyekundu MC .128 CCQ BOXER nyekundu  MC 857 CCU TVS nyekundu  na
T. 967  CKK  BOXER  nyeusi ambapo imebainika kuwa ni Namba bandia.

Pia,Jeshi hilo limefanikiwa kukamata nyara za serikali  huku likiwaasa
wananchi  kuchukua tahadhari dhidi ya wahalifu mbalimbali nchini
wakiwemo waendesha bodaboda nyakati za usiku.