Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na wanahabari leo Jijini Arusha wakati alipokabidhi kiasi cha Sh.Milioni tatu kwa Makocha wa wanariadha Alphonce Simbu na Failuna Abdu zilizotolewa na Shirikisho la Riadha Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya wanariadha hao ambao ndio watakaoliwakilisha Taifa katika mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika mwezi Juni mwaka huu huko Tokyo Japan.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe leo Januari 26.2020 amekabidhi kiasi cha Sh.Milioni tatu kwa Makocha wa wanariadha Alphonce Simbu na Failuna Abdu zilizotolewa na Shirikisho la Riadha Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya wanariadha hao ambao ndio watakaoliwakilisha Taifa katika mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika mwezi Juni mwaka huu huko Tokyo Japan.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Nyota FC Academy ya Jijini Arusha wakati alipotembelea uwanja wa Ngarenaro ambao umejengwa na Wadau wa Michezo kwa kushirikiana na Jiji hilo utakaotumiwa na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari leo Januari 26,2020.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza januari 26,2020 na viongozi wa Jiji la Arusha mara baada ya kukagua uwanja wa Ngarenaro Sports Complex uliojengwa na Jiji hilo kwa ajili ya matumizi ya michezo kwa shule za msingi na sekondari.
……………….
Na Shamimu Nyaki – WHUSM,Arusha.
Waziri wa Habari,Utaaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe amepongeza Jiji la Arusha kwa ujenzi viwanja vya michezo ambavyo ni vya kiwango cha juu vitakavyosaidia wanafunzi wa jiji hilo kuendeleza vipaji vyao.
Waziri Mwakyembe ametoa pongezi hizo leo Jijini Arusha alipokuwa akikagua Ngarenaro Sports Complex ambapo amesema kuwa jiji hilo linapaswa kuigwa na mikoa mingine kwakua michezo katika dunia ya sasa ni sekta ambayo inaleta ajira za kudumu.
“Arusha mmefanya kazi kubwa nawapongeza sana,najua wengi tunafahamu jinsi mkoa mkuu ulivyojijengea heshima katika mchezo wa riadha pamoja na Mkoa wa Manyara lakini hapa mmeenda mbali zaidi kuamua kujenga Complex hii hongereni sana”alisema Dkt.Mwakyembe.
Kwa upamde wake Mkurugenzi wa Jiji hilo Bw.Maulid Mgeni amesema kuwa Complex hiyo ni kwa ajili ya wanafunzi wa shule za Sekondari na Msingi za Serikali lakini iwapo shule binafsi zitahitaji kuutumia basi watapaswa kuchangia gharama nafuu.
“Complex hii ina viwanja vya netball,volleyball,soka pamoja na basketball lengo letu ni kuhakikisha vijana wetu wanakuza vipaji vyao hapa ili na wao waje kuwa nyota wakubwa baadae”aliongeza Bw.Maulid
Katika hatua nyingine Waziri Mwakyembe ameshauri wadau wengine wanaotaka kutengeneza viwanja vya michezo basi watumie nyasi za bandia ambazo hazihitaji gharama kubwa katika utunzaji na ameahidi kuiomba Serikali nyasi hizo zitakapokua zinaingizwa nchini ziweze kupata nafuu katika kulipiwa kodi.
Mhe.Waziri pia alikabidhi kiasi cha Sh.Milioni tatu kwa makocha wa wanariadha Alphonce Simbu na Failuna Abdu zilizotolewa na Shirikisho la Riadha Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya wanariadha hao ambao ndio watakaoliwakilisha Taifa katika mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika mwezi Juni mwaka huu huko Tokyo Japan.
Akizungumza bara baada ya kushuhudia makabidhiano hayo Bi Failuna Abdu ameahidi kufanya maandalizi kwa bidii ili akatangaze taifa vizuri kwakua anaamini watanzania wengi wapo pamoja na yeye na hatawaangusha.