Home Michezo YANGA SC USO KWA USO NA GWAMBINA FC 16 BORA AZAM SPORTS...

YANGA SC USO KWA USO NA GWAMBINA FC 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION CUP,YAICHAPA 2-0 PRISONS

0

Na.Mwaandishi Wetu

Timu ya Yanga SC imetinga hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho la Soka Tanzania ”maarufu kama Azam Sports Federetion Cup (ASCF) kwa kuichapa mbao 2-0 Tanzania Prisons kutoka mkoani Mbeya Mchezo uliomalizika kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Yanga ilianza kupata bao kupitia kwa  kiungo wao mpya Mghana, Bernard Morrisson kufunga bao la kwanza dakika ya tisa kwa penalti baada ya beki Michael Ismail wa Tanzania Prisons kuunawa mpira kwenye boksi katika harakati za kuokoa krosi ya Balama Mapinduzi.
Akitoa kwenye benchi kuchukua nafasi ya David Molinga , mshambuliaji kutoka Ivory Coast Yikpe Gislain Gnamien  aliyefunga bao la pili kwa kichwa dakika ya 64 akimalizika pasi ya kiufundi ya Bernard Morrison. 
Kwa ushindi huo, Yanga SC watamenyana na Gwambina FC ya Daraja la Kwanza ambayo jana iliitoa Ruvu Shooting kwa penalti 7-6 baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Gwambina, Misungwi.

Yanga SC inaungana na Alliance FC, Ndanda SC, Ihefu FC, JKT Tanzania, Simba SC, Gwambina FC na Sahare All Stars, KMC, Panama na Mbeya City kuingia raundi ya tano ya michuano hiyo ambayo bingwa wake hucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Hatua ya 32 Bora itahitimishwa kesho kwa mabingwa watetezi, Azam FC kumenyana na Friends Rangers Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Abdulaziz Makame, Deus Kaseke/Patrick Simomana dk82, Haruna Niyonzima, David Molinga/Yikpe Gislain dk57, Mapinduzi Balama na Bernard Morrison/ Feisal Salum dk98.

Tanzania Prisons: Jeremiah Kisubi, Michael Ismail, Benjamin Asukile, Vedastus Mwihambi, Nurdin Chona, Adilly Buha, Salum Kimenya/Samson Mbangula d68, Ezekia Mwashilindi, Jeremiah Juma/ Hamid Mohammed dk89, Paul Peter na Aziz Ismail/Cleophace Mkandala dk80.