Home Mchanganyiko RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AJUMUIKA NA VIJANA WA HALAIKI KATIKA HAFLA...

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AJUMUIKA NA VIJANA WA HALAIKI KATIKA HAFLA YA CHAKULA MAALUM ALICHOWAANDALIA VIWANJA VYA ZIWANI POLISI ZANZIBAR.

0

KATIBU wa Kamati ya Uhamasishaji na Halaiki Zanzibar .Ndg. Ali Mohammed Bakari (Shasha) akizungumza na kutowa shukrani kwa niaba ya Washiriki wa Halaiki ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar 12,January.2020, wakati wa hafla ya Chakula Maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya Vijana hao katika  viwanja vya Polisi Ziwani Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

VIJANA walioshiriki Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar,12.January.2020, wakipata chakula Maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) katika viwanja vya Polisi Ziwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa hafla ya Chakula Maalum kilichoandaliwa kwa Vijana walioshiriki Maashimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar , iliofanyika katika Viwanja vya Polisi Ziwani Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya Vijana walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Polisi Ziwani Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Katibu wa Kamati ya Uhamasishaji na Halaiki Zanzibar. Ndg. Ali Mohammed Bakari(Shasha) alipowasili katika viwanja vya Polisi Ziwani Zanzibar kuhudhuria hafla ya Chakula Maalum alichowaandalia Vijana wa Halaiki katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan 12,January 2020.(Picha na Ikulu).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama na Viongozi wa meza kuu wakati ukipigwa wimbo wa Taifa, (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Katika Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma.(Picha na Ikulu)

BAADHI ya Veteran wa Young Pioneer walioshiriki katika Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa, kabla ya kuaza kwa hafla ya Chakula Maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kwa Vijana wa Halaiki  walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika  Uwanja wa Amaan 12,January 2020, hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Polisi Ziwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)

BAADHI ya  Vijana walioshiki  katika Halaiki ya Madhimisha ya  Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar,12,January , wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili Mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) katika hafla ya Chakula Maalum alichowaandalia Vijana hao katika viwanja vya Polisi Ziwani Zanzibar.(Picha na Ikulu).