……………………………………………………….
Hafsa Omar-Dar es Saalam
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema mradi wa umeme wa Peri-Urban umebuniwa kwa mara ya kwanza nchini ili kukidhi haja ya ongezeko la mahitaji ya umeme kwa maeneo ambayo yanakua kwa kasi.
Ameyasema hayo,Januari 23,2020 wakati akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani,
Akizungumza na wanandishi wa Habari mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya ukaguzi wa mradi wa Peri-Urban mkoani humo, alisema,tangu mradi huo ulivyozinduliwa wananchi wameopokea vizuri na wameonesha muamko mkubwa wa kuunganisha na huduma hiyo.
“Imepita kipindi cha miezi minne tangu mradi huo uanzishwe tukaona kuna kila sababu ya kuja kukagua hali ya utekelezaji inavyoendelea ukizingatia mradi huu unagusa kama maeneo sita na ni mradi mkubwa kwasababu unatarajia kuunganisha wananchi wengi”
Alisema, wanamatumani kuwa ndani ya miezi mitano iliyobaki kazi zitaendelea vizuri na kwa kasi kubwa, kwakuwa vifaa vyote vinavyotekeleza mradi huo vingi vinazalishwa nchini, na kumtaka mkandarasi wa umeme kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza mradi kwa wakati.
Mgalu, aliwataka wasambazaji wa nguzo, nyaya na transifoma nchini kutumia fursa waliopewa na Serikali ya usambazaji wa vifaa hivyo, kuwasambaza vifaa hivyo kwa wakati na watoe ushirikiano kwa wakandarasi ili miradi yote iweze kumaliza ndani ya mda uliyopangwa.
Aidha, alisema mradi huo pia utasaidi sana Serikali kufikia lengo lake la kuwa ifikapo June 2021 vijjiji vyote viwe vimeunganishwa umeme na Wizara inamatumani makubwa kuwa lengo hilo litafikiwa kwa kupitia miradi mbalimbali kama REA 111, Peri-Urban na Ujazilizi
Naibu waziri pia aliwatoa hofu wananchi wote ambao wamelipia huduma ya umeme wa REA 111 mzunguko wa kwanza ambao kwenye idadi ya wateja wa awali walikuwa wamezidi idadi iliyopo kwenye mkataba wa mradi huo na kushindwa kuunganishiwa umeme kuwa wataunganishiwa na huduma hiyo mara tu baada ya mkataba ya nyongeza utakapoanza kazi.
“Hapa Kisarawe wapo wananchi takribani 239 walishalipa lakini walishindwa kuunganishwa kwa wakati kwasababu idadi iliyohitajika kwa kisarawe ilishakamilika kwahiyo sasa niwatoe hofu wote waliolipa na ambao hawajalipa kwamba unganishaji umeme utaanza na sasaivi REA wapo kwenye manunuzi ya vifaa”
Sambamba hayo, pia alieleza kuwa Serikali mwaka huu itaingia mkataba na wazalishaji binafsi kuzalisha umeme wa megawati 950 kutoka kwenye vyanzo vya upepo, jua na makaa ya mawe lakini pia kazi inaendelea ya utafiti wa chanzo cha umeme wa joto ardhi.