Na Farida Saidy Morogoro
………………………………..
Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo (Mb) amemtahadharisha mkandarasi anaejenga Kituo cha Daladala Manispaa ya Morogoro akisisitiza huenda akabomoa na kuanza kujenga Upya jengo la Utawala linalogharimu kiasi cha shilingi Milion 400 baada ya kutoridhiwa na hali ya utekelezaji wake.
Kituo cha Dalalada manispaa ya Morogoro utekelezaji wake unagharimu zaidi ya shilingi Bilion 5, fedha za mkopo toka benk ya Dunia, Unatekelezwa na mkandarasi mzalendo kampuni ya Nandra Constractin LTD ya Jijini Dar es salaam kukamilika kwake matarajio ni kuongeza wigo wa mapato kwa manispaa hii ya Morogoro.
Waziri Jaffo amefika kukagua mradi huu, ambapo wasiwasi wake ni muonekano wa jengo la Utawala akilinganisha na hali ilivyo katika maeneo mengine huku Makubaliano ni Mkandarasi kushirikiana na mhandisi mshauri kubomoa na kuanza upya kujenga jengo la utawala Utekelezaji wa makubaliano haya ni baada ya kukamilika kwa mradi.
Katika hatua nyingine, akiwa mkoani hapa waziri Jaffo amekagua na kuzindua shule mpya inayoelezwa kuwa ndio Shule ya Mfano , kwa shule za Sekondari za serikali nchini, shule ya Sekondari Mjimpya iliyogharimu kiasi cha shilingi Bilion 1.4.
Awali baadhi ya viongozi mkoani hapa wameeleza kuwa kupatikana kwa shule hiyo ya Mfano ni faraja kwao wao kama viongozi, ambapo dhamira ni kuongeza ushindani katika mitihani ya kitaifa na wakitamani shule hiyo kupanda hadhi kuchukua pia wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Shule ya sekondari Mji Mpya utekelezaji wake umegharimu kiasi cha Bilion 1 na million 400 fedha ambazo ni matunda ya Mradi wa Reli ya kisasa, shule hii inatajwa kuwa ndio shule ya mfano kwa shule zote za serikali nchini hususani ngazi ya kata, utekelezaji wake ukizingatia miundombinu ya wenye mahitaji maalum, maktaba ya kisasa na Maabara kwa masomo yote ya sayansi.