Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda Biashara na Mazingira Mhe. Kanali mstaafu Masoud Ally Khamis,akiwaongoza wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge wakati wa semina ya elimu iliyokuwa inatolewa na BRELA iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.
Kaimu Meneja Mkuu wa wakala wa usajili na leseni BRELA Bi. Roy Mhando akitoa elimu kwa wabunge akieleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na BRELA wakati wa semina elekezi iliyoandaliwa na BRELA kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda na Biashara iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa akitoa maoni yake kwa wabunge wa kamati ya viwanda, biashara na mazingira ambao walipewa elimu na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Hawa Mwaifunga (kushoto) akitoa maoni yake baada ya kupewa semina ya elimu kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ambapo waliitoa kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda Biashara na Mazingira iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akimsikiliza Naibu Waziri Mhe. Mhandisi Stellah Manyanya kwenye semina elekezi iliyoandaliwa na BRELA kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda na Biashara iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma.
Mbunge wa Monduli Mhe.Julius Laizer akichangia maada kwenye semina elekezi iliyoandaliwa na BRELA kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda Biashara na Mazingira iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe. Richard Ndasa,akitoa maoni yake wakati wa semina elekezi iliyoandaliwa na BRELA kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda Biashara na Mazingira iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Ndanda Mhe. Cecil Mwambe,akitoa maoni wakati wa semina elekezi iliyoandaliwa na BRELA kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda Biashara na Mazingira iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma kulia kwake ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Hawa Mwaifunga
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Lugha Bashungwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa semina elekezi iliyoandaliwa na BRELA kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda Biashara na Mazingira iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Kanali mstaafu Masoud Ally Khamis,akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa semina elekezi iliyoandaliwa na BRELA kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda Biashara na Mazingira iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Hawa Mwaifunga,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa semina elekezi iliyoandaliwa na BRELA kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda Biashara na Mazingira iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma.
Kaimu Meneja Mkuu wa wakala wa usajili na leseni BRELA Bi. Roy Mhando,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa semina elekezi iliyoandaliwa na BRELA kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda Biashara na Mazingira iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stellah Manyanya (kulia) akimsikiliza Kaimu Meneja Mkuu wa wakala wa usajili na leseni BRELA Bi. Roy Mhando (katikati)mara baada ya kumalizika kwa semina elekezi iliyoandaliwa na BRELA kwa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda Biashara na Mazingira iliyofanyika bungeni, jijini Dodoma.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa elimu ya majukumu yao kwa wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ili waone namna inavyotoa huduma kwa wananchi wake.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na BRELA. Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa kuhusiana na kazi na shughuli zinazofanywa na Wakala katika kutoa huduma kwa jamii bila kusahau changamoto mbalimbali zinazoikabili BRELA ili Kamati iweze kushauri.
Akitoa elimu hiyo kwa wabunge Kaimu Mtendaji Mkuu wa Brela Bi. Roy Mhando ameeleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na wakala ambazo ni kusimamia Sheria ya Makampuni Sura ya 212, sheria ya majina ya biashara sura ya 213, sheria ya alama za biashara na huduma, Sheria ya Usajili wa Hataza, Sheria ya Leseni za Viwanda, Sheria ya Leseni za Biashara.
Ameileza Kamati kuwa Wakala inafanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha inatimiza majukumu yake kwa ufasaha na kuwafikia wateja wake kwa kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Kanali mstaafu Masoud Ally Khamis amempongeza Kaimu Afisa mtedaji Mkuu wa Wakala kwa kazi nzuri anayoifanya na kuitaka Wakala kuendelea kutoa Elimu ili wadau wa biashara wajue huduma mbalimbali wanazotoa hasa katika maeneo ya pembezoni ambapo wadau wa biashara hawajui umuhimu wa kurasimisha biashara zao pia hawana uelewa wa matumizi ya Tehama.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amewashukuru Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa maoni na mawazo yao waliyoyatoa ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa ya kuongeza ufanisi kiutendaji katika kuwahudumia wananchi.
Aidha Mhe.Bashungwa ametoa maelekezo kwa BRELA kuwa waweke mkakati wa mawasiliano wenye lengo la kutangaza huduma zinazotolewa na Wakala kupita vyombo mbalimbali vya habari hasa kupitia redio za kijamii.
Baadhi ya wabunge waliotoa maoni ni pamoja na Mbunge wa Sumve Mhe. Richard Ndasa ambaye ameipongeza BRELA katika suala zima la kuwahudumia wateja kwani wamewawezesha wananchi wengi kupata huduma kwa urahisi kwani hivyo ndivyo inavyotakiwa katika kufikia uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.
Naye Mbunge wa Ndanda Mhe. Cecil Mwambe amewashauri BRELA wawe makini kwenye kazi za kila siku ili kuondoa malalamiko na changamoto wanazopata wateja hii itasaidia kuongeza idadi ya wateja na pato la Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Hawa Mwaifunga ameiomba BRELA wafike katika wilaya na Mikoa mbalimbali hapa nchi kwani huko kuna wadau wengi wanaohitaji kujua faida za kurasimisha biashara zao.
Mbunge wa Monduli Julius Laizer ameipongeza BRELA kwa kuandaa mfumo wao ambao wanaendelea kuuhuisha na akapendekeza ni vema taasisi zingine za biashara kuunganishwa pamoja.
Pia, amewapongeza watumishi wa BRELA kupitia kitengo cha TEHAMA wanaotoa msaada kwa wateja katika matumizi ya mtandao wa BRELA kwani wamekuwa wakisaidia sana wananchi pale wanapopata changamoto.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo amehitimisha kikao kwa kuwashukuru wajumbe wa kamati hiyo na kuwahimiza kuendelea kuishauri vema Serikali ili kuweza kufikia adhima ya Uchumi wa Kati unaongozwa na Viwanda ifikapo 2025.