yaliyojengwa na serikali kupitia TASAF kwa ufadhili wa OPEC katika kijiji cha Oldonyowas mkoani
Arusha.
wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (kushoto ) akiangalia zawadi iliyotolewa na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha kwa Ofisa Mwandamizi
wa OPEC Bwana Shams (katikati) baada ya kukagua miradi inayotekelezwa kwa ufadhili wa OPEC katika halmashauri hiyo.
wa OPEC kupitia mradi wa kupunguza umaskini katika kijiji cha Oldonyowas Mkoani
Arusha.
Arusha.
katika kijiji cha Oldonyowas mkoani Arusha wakiwa mbele ya majengo yaliyojengwa
na TASAF kwa ufadhili wa OPEC. Chini ni viongozi wa TASAF, halmashauri ya
wilaya ya Arusha wakimsikiliza Afisa Mwanadamizi kutoka OPEC wakati wa ukaguzi
wa majengo yaliyojengwa kwa ufadhili wa opec.
NA Estom Sanga- Arusha
Utekelezaji wa miradi ya kuondoa umaskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF-unaofadhiliwa na Umoja wa nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi Duniani- OPEC umepunguza kwa kiwango kikubwa adha ya watoto kwenda umbali mrefu kufuata huduma ya elimu katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Arusha.
Wakitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa
ujumbe wa Wataalamu kutoka OPEC, Wizara ya Fedha na TASAF, wakazi wa kijiji cha Oldonyowas ambao wamenufaika na miradi hiyo, wamesema ujenzi
wa miradi hiyo umeleta hamasa ya kupambana na umaskin na kuhamasisha wananchi kuwapeleka watoto wao shule.
Kupitia utaratibu wa ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa kuwashirikisha wananchi , Serikali kupitia TASAF kwa ufadhili wa OPEC imeweza kutatua tatizo lililokuwa
linawakabili wakazi wa kijiji cha Oldonyowas la uhaba wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, mabweni ya wanafunzi na matundu ya vyoo katika shule ya sekondari kijijini hapo.
Mafanikio hayo yameelezwa na uongozi wa kijiji hicho kuwa yameleta mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu ambayo kabla ya ujenzi wake haikuwa rahisi kwa watoto wa maeneo hayo kupata elimu ya sekondari kutokana na umbali wa kupatikana kwa huduma hiyo.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF pia umewezesha kupatikana kwa samani kwenye shule hiyo yakiwemo
madawati, viti na meza na hivyo kusaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la uhaba wa vifaa shuleni hapo na hivyo kuongeza ari ya walimu na wanafunzi katika masomo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amepongeza namna
wananchi wa maeneo hayo walivyoitikia mwito wa serikali wa kushiriki katika ujenzi wa miradi ya maendeleo jambo ambalo amesema limesaidia kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na ufanisi mkubwa.
Bwana Mwamanga pia ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuruhusu utekelezaji wa sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF, hatua ambayo amesema italeta mchango muhimu katika mapambano dhidi ya umaskini kama ambavyo
ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015 inavyoelekeza.
Kwa upande wake, mmoja wa maafisi waandamizi wa OPEC, Bwana Sharagim Shams amesema utekelezaji wa miradi ya TASAF ni ya kiwango kizuri hali iliyosababisha Umoja huo kukubali kuendelea kufadhili miradi ya kupunguza umaskini na kuboresha miundombinu hususani ya elimu nchini.
‘’nimevutiwa sana na namna ubora wa miradi tunayoifadhili ulivyo, tutaendelea kufanyakazi na serikali ya Tanzania kupitia TASAF’’ amesisitiza Bwana
Sharagim Shams.
Amewashauri Walengwa wa TASAF na wananchi wengine kutumia vizuri fursa hiyo hususani kwa kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata elimu kwenye shule zinazojengwa na TASAF kwa ufadhili wa OPEC ili kujenga raslimali watu iliyoelimika kwa siku zijazo.
Miradi inayofadhiliwa na OPEC kupitia TASAF inatekelezwa katika mikoa ya Njombe na Arusha . Miradi kama hiyo imekwishatekelezwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara nakiwa na lengo kuuu la kusaidia jitihada za wananchi na serikali kutatua changamoto za maendeleo ya wananchi na miradi ambayo
huibuliwa na wananchi wenyewe.