**********************************
Mwanaharakati huru nchini, Bw. Cyprian Musiba amewataka wanasiasa wasipende kupotosha Umma na kutishia amani ya nchi kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano huo Musiba amesema kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitaka nchi kuiingiza katika machafuko kuelekea uchaguzi ujao hivyo amewataka washughulikiwe ili kuondokana na machafuko katika kipindi hicho cha uchaguzi.
Aidha, Musiba ameshauri Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Magufuli kuendelea kuongoza nchi kwasababu kuna baadhi ya miundombinu haijakamilika aliyoipanga kuikamilisha katika uongozi wao.
“Tunamhitaji Mhe Rais Dkt John Magufuli kuliko kipindi chochote Tanzania, nawashauri watanzania kulinda Amani, na Umoja wetu, Vijana msikubali kudanganywa na walafi wa madaraka, tunahitaji utulivu wa akili na fikra kuelekea uchaguzi mkuu wetu wa mwezi wa 10 mwaka huu”. Amesema Musiba.
“Kuna watu wachache ambao wasiposhughulikiwa basi nchi yetu itaingia kwenye machafuko makubwa kwahiyo lazima wananchi hasa vijana amani ya nchi ipo mikononi mwenu epukeni vishawishi vyovyote kwa lengo la kuwagawa kwa makundi”. Amesema Bw.Musiba.