Farid Seif Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kadi Benki ya CRDB akipata huduma ya Chanja lipa Sepa iliyozinduliwa leo kwenye duka la Miniso lililoko Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo mteja anaweza kujinunulia bidhaa katika maduka yaliyoingia makubaliano na CRDB na kulipia fedha kwa Tembo Card Visa.
Farid Seif Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kadi Benki ya CRDB akizungumza katika duka la Miniso Mlimani City wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Antony Siyovelwa Meneja wa Kitengo cha kadi CRDB akifanya manunuzi kwa njia ya Tembo Card Visa katika duka la GSM Mlimani City jijini Dar es salaam leo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Antony Siyovelwa Meneja wa Kitengo cha kadi CRDB akiondoka na bidhaa zake mara baada ya kufanya manunuzi kwa njia ya Tembo Card Visa katika duka la GSM Mlimani City jijini Dar es salaam leo
………………………………………………………………..
Benki ya CRDB imezindua kampeni maalum ya matumizi ya kadi kufanya malipo ijulikanayo kama “Chanja, Lipa, Sepa” inayoendeshwa na Benki hiyo.
Farid Seif Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kadi Benki ya CRDB amesema Benki ya CRDB inayoongoza kwa ubunifu wa huduma na bidhaa katika soko, mnamo mwaka 2002 Benki ya CRDB ilizindua huduma ya TemboCard, ikiwa na lengo la kuwawezesha Watanzania na wateja wa Benki ya hiyo kupata huduma za kibenki kwa uharaka, usalama na unafuu. Uanzishwaji wa huduma ya TemboCard ulienda sambamba na uingizwaji wa vifaa maalum vya manunuzi (PoS) ili kuwawezesha wateja kufanya manunuzi katika sehemu mbalimbali kwa kutumia TemboCard zao.
Seif amesema kuwa Ili kuwapa wateja weke wigo mpana wa kufanya miamala, CRDB imeungana na mashirika ya kimataifa ya huduma za malipo ikiwamo Visa International ambapo mteja anaweza kufanya malipo popote pale duniani ikiwamo kwenye maduka ya mtandaoni.
Ameongeza kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana Benki ya CRDB ilifanikiwa kuingiza jumla zaidi ya TemboCard milioni 2 sokoni, ambapo kwa sasa ina wastani wa miamala 50,000 ya malipo kwa njia ya kadi kwa mwezi. Haya ni mafanikio makubwa na ya kujivunia sana.
Pamoja na mafanikio hayo makubwa, wateja wengi bado hawana utamaduni wakutumia TemboCard zao kufanya malipo, kitu ambacho kinawapelekea kukosa baadhi ya huduma.
Hivyo Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Visa International inazindua kampeni maalum ya kuwahamasisha wateja na watanzania kwa ujumla kutumia kadi zao kufanya malipo, kampeni ambayo imepewa jina la “Chanja, Lipa, Sepa”.
“Ili kushiriki katika kampeni hii mteja anatakiwa kutumia kadi yake ya TemboCardVisa au huduma ya SimBankingVisa (QR Code) kufanya malipo ya manunuzi katika supermarkets, maduka ya rejareja, migahawa, bar, hoteli na sehemu mbalimbali zinazopokea malipo kwa njia ya kadi au QR Code ikiwamo mtandaoni”.Amesema Farid Seif
Kupitia kampeni hii ya “Chanja, Lipa, Sepa”, wateja watakao fanya malipo kwa TemboCardVisa na SimBankingVisa wataweza kufurahia punguzo la bei hadi asilimia 60 kwa manunuzi ya kuanzia shilingi 30,000 katika maduka na migahawa mbalimbali.
Ameyataja baadhi ya maeneo ambayo wateja wa TemboCardVisa na SimBankingVisa wataweza kufurahia punguzo kwa upande wa maduka kuwa ni ;
- GSM Mlimani City na Mikocheni
- Orca deco
- Miniso Mlimani City/ Aura
- MM brands
- Baby shop – Mlimani City/ Pugu
- Splash – Mlimani City/ Msasani
- Mr Price – Mlimani City/ Aura
- Little More
- Cons collection
- Tanzania brand eyes
- Shoe express n.k
Amesema maeneo mengine ambayo wateja watafurahia punguzo (discount) ni pamoja na Tips Kidimbwi, The Luxe, Gorvenors, The Boardrooms n.k. Mbali na kupata punguzo, wateja pia watakuwa wakipata zawadi za papo kwa papo pindi watakapofanya malipo ikiwamo T-shirts, kofia, Key-holders na zawadi nyengine nyingi.
Amewaomba wateja wote wa Benki ya CRDB wanaotumia TemboCardVisa na SimBankingVisa kufanya malipo yao ya manunuzi kwa huduma hiyo ya kidijitali . Lengo llikiwa ni kuona Watanzania wanaondokana na matumizi ya pesa taslimu na kutumia mifumo hii ya kidijitali ambayo ni rahisi, salama na nafuu kufanya malipo.
Amemaliza na kusema Kwa wale ambao bado hawana akaunti Benki ya CRDB, huu ndio wakati wakufungua akaunti na kupata TemboCardVisa na kujiunga na huduma ya SimBankingApp ili waweze kufurahi SimBankingVisa.